Samsung imepata mfanyakazi mpya, mfanyakazi huyu kwa zamani alikua anafanya kazi katika kampuni ya Mercedes.
Hubert H. Lee, anakua na kazi ya kuiongoza timu nzima ya ubunifu wa simu janja ambayo inajulikana kama MX (Mobile eXperience) Design ambayo ni kitengo kimojawapo cha Samsung.
Kwa mara ya kwanza Lee alikua mkuu wa kitengo cha ubunifu cha Mercedes kwa upande wa china lakini kwa sasa anakua na cheo katika kampuni ya Samsung.
Kingine ni kwamba bwana Lee anasifika sana kwa utendaji wake wa kazi na pia ana tuzo nyingi sana kutoka marekani na hata china ambazo zinaonyesha kuwa wadau mbalimbali wanatambua uwepo wake.
Samsung kama kampuni wanasifika sana kwa kubuni na kutengeneza bidhaa ambazo ni nzuri kwa muonekano na hata kwa ufanyaji wake wa kazi.
“Najivunia kujiunga na kampuni ambayo iko mstari wa mbele kabisa kwa ubunifu katika soko la simu janja na kwa pamoja tutaendeleza ubunifu wa hali ya juu” – Lee.
Bwana lee ataongoza timu nzima ambayo inaandaa ubunifu katika vifaa vya S Series, Z Series, Galaxy Tab, Galaxy Watch na vifaa vingine vingi
Ni wazi kabisa kulingana na bidhaa hizo na ubunifu wa hali ya juu kutoka Samsung ambao umetumika unaina kabisa kwamba bwana Lee atakua na kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha kuwa kampuni inabaki kuwa juu katika ubunifu.
Toleo la Samsung s23 linatoka mwakani kwenye miezi ya mwanzo mwanzo kabisa na ni wazi kwamba kuna hati hati kubwa kuwa hahusiki kwa ubunifu huo kwani ukiangalia muda ambao kajiunga na kampuni na muda ambao toleo hilo litatoka ni mdogo sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani bwana Lee na timu yake mpya wataweza kuleta ubunifu wa hali ya juu kabisa kwa vifaa vijavyo kutoka Samsung.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.