fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Blackberry simu

Blackberry Kuwapumzisha Kazi Wafanyakazi 200, Akiwemo Aliyebuni BBM!

Blackberry Kuwapumzisha Kazi Wafanyakazi 200, Akiwemo Aliyebuni BBM!

Spread the love

Simu ya Priv katika Blackberry inaweza ikawa kama vile iPhone kwa Apple – huwezi jua labda inategemewa kiasi hicho – lakini hata hivyo ni bado mapema sana kujua kwa uhakika kama simu moja inaweza kuliokona kampuni hili kutoka Canada

Kuokoa kampuni ya BlackBerry inabidi ufanyike ubunifu wa hali ya juu.

Ukiachana na kuzindua simu janja yao ambayo ilisubiriwa kwa hamu, kuwakata (kuwapumzisha) baadhi ya watu katika kampuni hiyo ni moja kati ya plani zao

Mijadala kibao imetokea , wengi wanasema simu mpya za BlackBerry zinaweza zikawa simu za kwanza za Android ambazo zina ulinzi wa hali ya juu kishinda zote. Taarifa zilizopo ni kwamba simu hii inauza katika baadhi ya masoko duniani.

SOMA PIA  Facebook na Cambridge Analytica zaburuzwa mahakamani

Licha ya kwamba miaka kadhaa iliyopita ilionekana dhahiri kuwa Blackberry yenye program endeshaji ya android ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. Muda huo umepita na sasa ni wakati wa Blackberry wa kuionyesha dunia maajabu yake, huku ikionekana bila ubishi ya kwamba wanaweza kupata mafanikio wakitumia programu endeshaji ya Android.

Blackberry Priv

Blackberry Priv

Lakini mkurugenzi mkuu wa Blackberry Bw. John Chen amesema wazi kuwa kampuni hiyo inahitaji kuuza simu milioni 5 tuu ili kujihakikishia kubakia katika soko hilo. Kama hilo halitafanikiwa basi kampuni hilo litaachana kabisa na biashara ya kutengeneza simu na kuuza na kujidhatiti katika biashara ya programu spesheli (software), hasa za ulinzi.

SOMA PIA  Google Pixel 5a 5G itatoka mwaka huu

Mpaka muda huo ufike inaonekana kampuni ya Blackberry inafanya mambo mengine katika ofisi zake. Kampuni imewapumzisha mamia ya wafanyakazi – hii ni namba ndogo sana katika kampuni kama hii – kati ya wale waliopumzishwa, miongoni mwao yupo mkurugenzi wa usanifu, Bw. Gary Klassen.

Kumbuka Bw. Klessen yeye ndio nyuma ya utengenezaji wa BBM ambayo ilipendwa na wengi. BBM ni huduma ya meseji kutoka katika simu za BlackBerry

Kampuni ya BlackBerry pia imekanusha taarifa zilizoenea kwamba asilimia 35 ya nguvu kazi katika kampuni itakuwa haina kazi. Lakini kampuni hiyo inasema watu waliopumzishwa ni namba ndogo sana ya wafanyakazi katika kampuni hiyo.

SOMA PIA  Kosa la kiusalama katika iPhone 6s lagunduliwa

Kwa usahihi kabisa BlackBerry imewapumzisha kazi wafanya kazi 200. Inaonekana dhahiri kuwa Bw. Chen anataka kuweka akili yake yote katika program endeshaji ya android. Ukichana na Priv, Blackberry inategemewa kuachia simu zingine mbili za Android ambazo zitakuwa za bei rahisi kidogo kulinganisha na Priv.

Tuzisubirie simu hizi ili tuone Android ndani ya BB.Ningependa kusikia kutoka kwako je ni sahihi hii ni namba ndogo kama wanavyosema  wenyewe? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Tembelea Teknokona kila siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania