fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Infinix Kamera Picha simu Smartphones

FAHAMU: Ujio Wa Infinix Zero X, Simu Ya Kwanza Kupiga Picha Za Anga!

FAHAMU: Ujio Wa Infinix Zero X, Simu Ya Kwanza Kupiga Picha Za Anga!

Spread the love

Baada ya tovuti mbalimbali maarufu kama GSMArena, XDA Developers kuandika makala ya uzinduzi wa Infinix ZERO X na kutupia Picha…

… Inayoashiria ni kamera za Infinix ZERO X nyuma ikiwa na kamera 3 na kwa inavyosemekana kamera kuu ni MP108 OIS Ultra Resolution. 

Muundo Wa Kamera Na Flash Katika Simu Ya Infinix Zero X Pro Ukiwa Unaonyesha Baadhi Ya Sifa Za Kamera Hiyo

Muundo Wa Kamera Na Flash Katika Simu Ya Infinix Zero X Pro Ukiwa Unaonyesha Baadhi Ya Sifa Za Kamera Hiyo

Bado haijatosha wataalamu wa maswala ya nyota na mwezi ‘Royal Observatory Greenwich’ ambao ni washirika na Kampuni ya simu Infinix katika kuileta Infinix ZERO X nao wameonekana kusifia zaidi teknolojia ya 60X periscope zoom lens ya Infinix ZERO X.

Wataalamu hao wa nyota (Astronomers) wanadai baada ya tafiti waliyofanya wamebaini  kuwa 60X periscope Zoom Lens ya Infinix ZERO X inauwezo wa kupiga picha za Anga kama mwezi n.k 

Sifa hizo zimeonekana kuwachanganya wadau wa simu za Infinix katika nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambapo simu hii bado kuzinduliwa.

Shauku ni kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji je simu hii itatua lini Bongo na je itakuwa na sifa sawa na hii inayoonekana kusifiwa zaidi mitandaoni?

Picha Ya Mbele Na Nyuma (Simu Ya Infinix Zero X Pro)

Picha Ya Mbele Na Nyuma (Simu Ya Infinix Zero X Pro)

Kampuni ya simu Infinix bado haijaongea rasmi kuhusu hili isipokuwa dalili ya mvua ni mawingu kwani kupitia @infinixmobiletz kunaashiria ujio wa kitu kipya.

Hebu tukae mkao wa kula huku tukisubiria tamko kuu kutoka kwa kampuni ya Infinix, vile vile usisahu kuchungulia katika mitandao yao ya kijamii maana siku yeyote unaweza ukashangaa wanatoa mzigo.

Niambie hii Kutoka kampuni ya simu ya Infinix Umeipokeaje? je ulishawahi fikiria kama simu inaweza kupiga picha za anga?

Vile vile hivi umesikia fununu zingine zozote kuhusu simu hii?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

SOMA PIA  iPhone SE 2020 imetoka baada ya fununu nyingi
Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania