fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Mtandao wa Kijamii Zoom

Zoom Yainunua Kampuni Inayofanya Tafsiri Za Papo Kwa Papo!

Zoom Yainunua Kampuni Inayofanya Tafsiri Za Papo Kwa Papo!

Spread the love

Zoom imetangaza kupitia mtandao wake kwamba imenunua kampuni ya kijerumani inayojulikana kama Karlsruhe Information Technology Solutions au kwa namna nyingine Kites GmbH.

Kampuni hii inajihusisha sana katika maswala ya tafsiri za papo kwa papo na pia Zoom inasema kuwa itaihusisha huduma hiyo kwenda sambamba na huduma yake ya kurahishisha mawasiliano baina ya watu na watu.

Mtandao Wa Zoom

Mtandao Wa Zoom

Kwa namna nyingine ni kwamba mtandao utakua na uwezo wa kutafsiri lugha za watu amabo wanaongea lugha tofauti na hasa hasa katika kipengele chake cha maongezi ya video ya watu wengi (video conferencing).

Kites ilianzishwa rasmi ikiwa na lengo kuu la kuwasaidia wanafunzi wa chuo darasani katika tafsiri za kiingereza na kijerumani kulingana na lugha ambazo maprofesa wao wanafundishia.

Mpaka sasa mtandao wa kijamii wa Zoom una huduma ya unukuzi (transcription) wa papo kwa papo lakini kwa sasa huduma hii ni kwa wale tuu ambao wanafanya mazungumzo kwa kutumia lugha ya kiingereza.

 Zoom

Zoom

Katika Unukuzi bado Zoom wanakubali kwamba kuna baadhi ya madhaifu yapo na wapo tayari katika kufanya mipango ili kuona ni namna gani ambayo wanaweza boresha huduma hiyo.

SOMA PIA  WhatsApp haina chanzo cha kuingiza Pesa mpaka sasa #Uchambuzi

Aidha Zoom wanasema kuwa mchakato unaofuata ni kuhakikisha kuwa wanafungua ofisi nchini ujerumani ili kufanya kazi na wafanyakazi wa Kaites moja kwa moja

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, wewe hili umelipokea vipi?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania