fbpx

Obama na mkewe wapo kwenye mazungumzo na Netflix, kuja na Shows

0

Sambaza

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama na mkewe wapo kwenye mazungumzo na Netflix ya kuja na kipindi chao spesheli kupitia tovuti maarufu ya burudani za video – Netflix.

Katika taarifa iliyovuja kabla ya muda wake kupitia tovuti ya New York Times, inaonesha mazungumzo hayo bado yanaendelea na yatahusisha Bwana Obama na mkewe, Michelle, kuja na vipindi vyao vya kitofauti na vitakavyoweza kupatikana kupitia mtandao wa Netflix tuu.

Obama na mkewe wapo kwenye mazungumzo na Netflix

Obama na mkewe wapo kwenye mazungumzo na Netflix

Inasemekana Obama hana lengo la kutumia vipindi hivyo kumponda Rais wa sasa Marekani, Bwana Trump, bali yeye na mkewe watakuja na vipindi vya kuleta hamasa za kimaendeleo kwa watu – kiuchumi, kiteknolojia n.k.

Mtandao wa Netflix una watumiaji zaidi ya milioni 100 duniani kote, na kupitia mtandao huo kuna vipindi vya aina mbalimbali – muvi, tamthilia n.k.

Wengi wanaamini uamuzi huu utawaletea wakina Obama pesa nyingi zaidi, hadi sasa tayari yeye na mkewe wana mkataba wa zaidi ya dola milioni 60 za Marekani katika uandikaji wa vitabu.

Obama ni moja ya marais wenye followers wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii, Facebook ukurasa wake una Likes milioni 55, wakati Twitter anafollowers milioni 101.

Je una fahamu mangapi kuhusu tovuti ya kustream movi, tamthilia n.k ya Netflix? Soma zaidi hapa makala kuhusu Netflix -> Teknokona/Netflix

Chanzo: NYTimes

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.