Ni wazi kuwa mitandao mingi ya kijamii inatumia huduma ya handles (@) lakini kwa mtandoa wa Instagram kwa muda mrefu imekua nyuma maana wao kwa muda walikua na mentions tuu.
Kingine hii kwa wale ambao ni waandaji wa maudhui (Katika mtandao wa Youtube) itakua ni vizuri sana kwao maana itakua ni njia rahisi sana katika utambuzi wao kwa jamii – au hata wao baina ya wao
Cha msingi hapa na cha kutofautisha ni kwamba inabidi watu wajue kwamba kuna utofauti mkubwa baina ya Mention, Handles na hata jina la URL.
Cha kujua ni kwamba akaunti zote za mitandao ya kijamii zina URL (ile ambayo unaikuta au hata ambayo umeiweka wewe).
Huduma hii ya handles itaanza kupatikana dunia nzima tarehe 14 oktoba ya mwaka huu, hivyo usishangae kutupata katika mtandoa wa Youtube tukiwa tunapatikana kama @Teknokona yaaani www.youtube.com/@teknokona.
Uzuri wa handles ni kwamba waandaji wa maudhui wanaweza wakawatag waandaaji wa maudhui wenzao katika vichwa vya habari n.k (fikiria kama wakiwa wameshirikiana katika kuandaa maudhui pamoja n.k)

Kama mpaka tarehe 14 ya mwezi huu waandaaji wa maudhui watakua hawajaweka handles zao basi Youtube yenyewe itawawekea ambayo wanadhani kulingana na channel zao.
Kama hili likitokea au likikufika basi unaweza kubadilisha Handle hiyo kupitia www.youtube.com/handle na kuweza kubadilisha handle kwenda ile unayoitaka.
Kingine ni kwamba mtandao wa Youtube unadai kuwa kama ukurasa Fulani wa youtube umetengenezewa URL (na muandaaji maudhui mwenyewe) muda mwingi mtandao utabadilisha hiyo na kuwa handle ya akaunti hiyo
Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe ni muandaaji wa maudhui katika mtandao wa kijamii wa Youtube? Niambie hili umelipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.