Intel ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa yanayojihusisha na maswala ya kompyuta na vifaa vingine vingi vya kielektroniki ambayo inafanya vizuri sana katika soko.
Ukaichana na ukubwa wake na ufanyaje wake vizuri katika soko kwa muda mrefu lakini bado vyanzo mbalimbali kama the verge vinasema kuwa kampuni ina mpango kupunguza ajira nyingi.
Hali hii ni wazi wazi kuwa itapunguza kazi nyingi sana katika kampuni, na pengine hili linaweza bainika ndani ya mwezi huu huu.
Kitu ambacho unaweza ukawa unajiuliza kwamba ni kwanini hili linaweza likatokea, hapa unaambiwa kwamba kampuni imeshuka sana kimauzo.
Mauzo ambayo yanaongelewa hapa ni mauzo yale ya chip (mpaka zile ambazo zinatumika katika komyuta).
Taarifa ambazo zipo ni kwamba uamuzi huo utawaathiri sana wale wafanyakazi ambao wapo katika kitengo cha mauzo na masoko.
Kingine ni kwamba, kwa hali liyopo sasa hivi inaeleweka kuwa kwa makampuni mengi hali ni mbaya, na haswa kutokana na swala zima la mfumuko wa bei na makampuni mengi yanaona sehemu ya kuponea mara nyingi ni kupunguza matumizi na watu.
Makampuni mengi ya kiteknolojia tangia mwaka huu uanze yameonekana yakipunguza watu na sio kwa Intel peke yake katika hili.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kupunguza ajira ndio suluhu ya makampuni haya kufanya vizuri kimapato?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.