Kampuni ya magemu ya Nintendo ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa kuwahi kutokea katika soko la magemu kwa sasa imeziweka pembeni.
Hapa ni kwamba kinachofanyika ni kwamba kampuni ya Nintendo imeacha kabisa kutoa ruhusa ya watu ku’log in kwa kupitia mitandao ya Twitter na Facebook.

Hautaweza kuingia katika akaunti yako ya mtandao huo wa gemu kwa kutumia akaunti hizo katika mitandao hiyo miwili ya kijamii.
Mpaka kufikia oktoba 25 mwaka 2022 jambo hili halitawezekana kabisa
As of 10/25/2022, it will no longer be possible to sign in to a Nintendo Account using a Facebook or Twitter account. We apologize for any inconvenience.
More info on signing in from 10/25/2022:https://t.co/hxcwFP1O9s
— Nintendo of America (@NintendoAmerica) September 20, 2022
Lakini kwa wale ambao wanatumia akaunti ya Google au hata Apple wataweza kutumia akaunti hizo kuingia katika akaunti yao ya gemu hiyo.

Aidha kampuni imesema kuwa hata kutengeneza akaunti mpya za gemu hiyo kwa kupitia Facebook na Twitter, jambo hilo halitawezekana tena.
Soma kila kitu kuhusiana na Nintendo >>HAPA<<

Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kuwapunguza watu kwa namna hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.