Moja kati ya mitandao iliyokua kwa kasi kabisa na kuishangaza dunia ni mtandao wa TikTok, na kama ni mtu wa mitandao ya kijamii nina uhakika ushawahi kukutana na comment ambayo hujaipenda.
Je ukikutana nayo huwa unafanya nini? Ukiachana na kusikitika au kusonya? Kwa taarifa yako kipengele cha kuonesha dhahiri kama hujapendeza na comment katika mtandao wa TikTok Kilikuwepo muda tuu..
..Ndio kilikuwepo muda tuu ila ni kwa watu wachache ambao walikua wamechaguliwa, kwa sasa kinaachiwa na kutumika na dunia nzima.

Kampuni inafanya hivi katika kuhakikisha kuwa mtumiaji wa mtandao huu anapata kile kilicho bora wakati akiwa anatumia mtandao huu wa kijamii.
Kingine kizuri ni kwamba kwa kutumia kipengele hichi inaweza ikawa ni rahisi sana kwa mtandao kuwezo kuchukua hatua dhidi ya watumiaji ambao wanakiuka baadhi ya sharia za mitandao kama vile lugha za matusi.
Kinachofanyika hapa ni kama unavyoona katika mtandao wa kijamii wa Youtube, ukiingia katika eneo la comment katika mtandao huo lazima utaona vialama vya kupenda(like) au dislike (kutopenda) pembeni ya comment zilizopo.

Hivyo sio jambo jipya sana katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii ila lina mashiko makubwa katika mtandao wa TikTok, maana saa zingine comments huwa zinakua na mambo mengi kuliko hata maudhui ambayo yametumwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani kipengele hicho ni cha msingi sana katika mitandao ya kijamii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.