Kuna muda una mengi ya kuongea katika mtandao wa kijamii lakini unaishia kusema kwa uchache kulingana na uchache wa maneno ambao umewekwa katika mtandao husika, kwa upande wa Twitter blue kidogo hili limebadilika.
Twitter Blue ni huduma ya Twitter ambayo ni ya kulipia na inakua na utofauti kidogo ukilinganisha na Twitter ya kawaida.
Kwa mara ya kwanza kabisa Twitter blue ilikua inaruhusu maneno 280 tuu lakini kwa sasa idadi ya namba hiyo imepanda mpaka kufikia 4,000.
need more than 280 characters to express yourself?
we know that lots of you do… and while we love a good thread, sometimes you just want to Tweet everything all at once. we get that.
so we're introducing longer Tweets! you're gonna want to check this out. tap this 👉… https://t.co/lge9udRzLE
— Twitter Blue (@TwitterBlue) February 8, 2023
Hii itakua hivi kama uki’tweet kwa maneno 4,000 kaa ukijua yataonekana maneno 280 tuu na kisha mbele yake kutakua na neno “Show more” ili kuendelea kusoma zaidi.
Twitter ni moja kati ya mtandao wa kijamii ambao umekumbwa na mabadiliko mengi baada ya kupata mmiliki mpya na bado inaonekana yataendelea tuu.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Twitter >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako,niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni sawa kwa mtandao wa Twiiter Blue kuongeza maneno yake.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.