fbpx
Mtandao, simu, Teknolojia

Wanafunzi Wanafanya Vizuri Katika Shule Ambazo Zinakataza Simu!

wanafunzi-wanafanya-vizuri-katika-shule-ambazo-zinakataza-simu
Sambaza

Hivi ushawahi fikiria kama simu inaongeza upeo wa kufikiri wa mtoto? Mjadala unaweza zuka juu ya jambo hili lakini bado ukweli utabaki pale pale haziwafanyi wawe na upeo mkubwa. Pengine labda zinawafanya wawe na upeo mkubwa katika Snapchat, WhatsApp, Instagram na kwenye magemu na mitandao mingine mingi ya kijamii.

Utafiti Mmoja unapinga kabisa na unatoa ushahidi kwamba matumizi ya simu kwa mwanafunzi kipindi awepo shuleni kunamwongezea mwanafunzi sababu ya kufeli.

 

utumiaji wa simu darasaniUtafiti huu umefanywa na taasisi ya London School of Economics utafiti huu ulionyesha kuwa katika shule ambazo zinakataza matumizi ya simu kwa wanafunzi zinafanya vizuri zaidi ya zile ambazo hazikatazi. Utafiti huo ulipewa jina la Ill Communication: Technology, Distraction & Student Performance ( Faili hili ni la mfumo wa PDF). Utafiti huu ulifanyiaka katika majiji manne huko wingereza na kutoa majibu kuwa ni wale tuu wanaotumia zawadi zao walizopewa na mungu (akili binafsi) ndio wanafanya vizuri kuliko wale ambao wanatumia simu.

INAYOHUSIANA  WhatsApp yaleta kipengele kipya kwenye makundi #Masasisho

Hapa katika huu uchunguzi watafiti hawakupata shida sana maana waliangalia kipindi ambacho simu zilikua zinaruhusiwa pale shuleni na kipindi zilipokatazwa na kufananisha ufaulu wa vipindi hivyo viwili.

Utafiti huu una ukweli mkubwa ndani yake kwa kuwa ukuaji huu mkubwa wa teknolojia una athiri maendeleo kwa kiasi kikubwa kwani teknolojia nyingi kwa sasa zimekuwa kama ni moja kati ya vile vitu ambavyo vinamuondoa mtu katika kufanya shughuli za kimaendelea na kuanza kutumia teknolojia hizo, mfano simu za mkononi

INAYOHUSIANA  Oppo yashehrekea pamoja na uzinduzi wa bidhaa

Sio kwamba watu wazima na wenyewe simu haziwapotezei mda na kuwaweka nje ya reli katika shughuli za kimaendeleo, hata wao zina waathiri kwa kiasi kikubwa tuu. Tunakaa kwenye mabasi, treni hata katika mikutano na shughuli zingine na tunagundua vitu mbali mbali kupitia simu zetu za mkononi — mfano ile video ya yule simba anaecheka  kwa takribani dakika tatu — mda ambao umetumika kuona hiyo video pengine kuna jambo lingine chanya lingefanyika

INAYOHUSIANA  Nanowires: Watafiti wagundua njia ya kufanya Mabetri kudumu muda mrefu zaidi!

Sawa bila simu zetu pengine hatuwezi fanya kitu, lakini zikizuiliwa mashuleni ufaulu wa wanafunzi utaongezeka. Tuambie nini kingine kunachihusu teknolojia ukiachana na ile ya simu kinasababisha kufeli kwa wanafunzi. Tembelea kurasa zetu zingine pendwa za  Twitter, Facebook Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*