Wengi wetu ambao tunapenda kwenda na wakati na kutotaka kupitwa na yanayoendelea ulimwenguni tumejikuta tukitumia muda mwingi kushika simu zetu tukizitumia kwa mambo mbalimbali haswa mawasiliano na kupata habari. Najua pia wengi wetu hupenda kwenda kwenye migahawa kupata chakula huku tukiendelea kuwa karibu na simu zetu muda wote.
Sasa imagine umekwenda kwenye mgahawa na umenunua chakula chako ambacho kinahitaji zaidi kutumia mikono katika kula halafu meseji muhimu inaingia unaijibu vipi na umeshashika chakula? Najua utataka umalize chakula haraka unawe mikono ndio ushike simu kujibu meseji. Kwa kiasi flani inakera hii.
Mgahawa maarufu duniani KFC katika harakati zake kuwavutia wateja na kuongeza soko la vyakula vyake uliamua kushirikiana na kampuni moja ya teknolojia huko Ujerumani kutengeneza Trei Keyboard za kubebea chakula ambazo pia hufanya kazi kama keyboard hapo hapo.
Trei hizo zenye Keyboard ambazo unaweza kuzichaji ni nyembamba na nyepesi kiasi cha kuweza kuzikunja kama gazeti zina uwezo wa kuwasiliana na simu janja(smartphone) kwa kutumia Bluetooth pale unapoziwasha. Hii huziwezesha kuwa keyboard mbadala wa keyboard ya simu kwahiyo meseji inapoingia huhitaji hata kugusa simu yako kwani unaweza kuandika meseji kupitia Trey hizo hivyo kuepusha kuichafua simu na mikono iliyoshika chakula. Trey Typer Keyboard hizi baada ya kuwekwa katika migahawa ya KFC, zote zilichukuliwa na wateja walioonyesha kuvutiwa nazo sana.
Je, tutegemee kuziona katika migahawa ya KFC iliyopo hapa nchini? Na hii ndio raha ya teknolojia.
Nitafrah zkifka bongo.. kw wat wasaf km cc ttazifrahia..