Inaonekana Instagram imegundua ya kwamba kuna wanaokosa kuziona baadhi ya picha bora zinazotumwa kila siku na akaunti wanazozifuatilia na hivyo kuanzia sasa wataanza kutuma barua pepe kwa watumiaji wake kuwakumbusha. Barua pepe hizi zitakuwa zinakujia kila siku.
Teknolojia ya barua pepe bado ni moja ya teknolojia inayotumika zaidi kwa wakazi wengi wa nchi zilizoendelea na baadhi ya watu wengi katika nchi zinazoendelea kama zetu. Na wanategemea uhamuzi huu utasaidia kuwakumbusha watu kuzidi kutembelea akaunti zao za Instagram, na pia kutopitwa na picha ambazo zinafanya vizuri zaidi katika akaunti zile wanazofuatilia.
Kwa kiasi kikubwa uamuzi huu unaonekana ni kwa ajili ya kuzidi kuhakikisha watumiaji wake hawaisahau.
Kuanzia sasa tegemea kupata barua pepe angalau moja kila siku kutoka Instagram ikikukumbusha picha zilizofanya vizuri na wanazodhani wewe pia ungevutiwa nazo. Hii pia inaweza ikasaidia hasa kama wewe unafuatilia akaunti nyingi sana kwani inawezekana muda unaoingia ikawa picha na habari ambazo pia zingekuwa nzuri kwako zishapita.
Instagram imekua kwa kasi sana, mwaka jana tuu inasemekana ilifanikiwa kukua kwa kasi zaidi ukiacha mtandao kama wa Twitter nyuma kabisa katika kasi ya ukuaji.
Soma Pia; Instagram yaipita Twitter Kwa Ukubwa: Mabadiliko Yanakuja!
No Comment! Be the first one.