fbpx

Android, apps, Google, Teknolojia

Kutumia kalenda za Google kutunza kumbukumbu

kutumia-kalenda-za-google-kutunza-kumbukumbu

Sambaza

Waswahili husema “Mali bila daftari huisha bila habari“. Msemo huu unatukumbusha kuwa ili mambo yaweze kwenda sawia basi hatuna budi kutunza kumbukumbu na kuwepo kwa teknolojia vitu vinaweza kukamilika kidijiti tuu.

Kwa wale ambao tumekuwa na uraibu kwenye mambo mbalimbali ya teknolojia tunajikuta tukitumia vifaa vya kidijiti ili kuepuka matumizi ya karatasi, kuokoa muda. Na utakubaliana na mimi kuwa simu janja zeu zinaweza kutufanya tukatunza mambo mengi mbali na kutuma ujumbe, kupiga/kupokea simu.

Katika jambo ambalo limenifurahisha ni uamuzi wa Google kuwezesha mtu kuweka kumbukumbu ya vitu mbalimbali mathalani mkutano, siku ya kuonana na daktari, n.k ndani ya kalenda za Google kwenye Android/iOS. Utakubaliana na mimi kuwa kabla ya maboresho hayo ilimladhimu mtu kuweka kumbukumbu ya vitu anavyopaswa kufanya (to-do list) kwa kutumia programu tumishi husika na si kwenye kalenda; hilo sasa limefikia ukomo.

INAYOHUSIANA  Google yaongezwa kwenye SwiftKey
kutunza kumbukumbu
Sasa unaweza kutunza kumbukumbu ya vitu vya kufanya ndani ya kalenda.

Kwa hakika simu janja zimepunguza masuala ya kutembea na vitu vya kuandika mabo madogo madogo kwani shughuli hiyo inaweza kufanya vyema kabisa kwenye rununu sehemu yoyote na wakati wowote kuanzia kwenye uandaaji, uhariri na hata ikibidi kumtumia mtu/kumshirikisha mwingine hayo yote yanaweza kufanyika kwa ufanisi kabisa.

TeknoKona inaamini makala hii imekupa somo la kuwa mtu atakayependa kuweka ratiba yake katika mfumo wa kidijiti na bila shaka utakuwa mwalimu kwa wengine.

Chanzo: Engadget

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*