fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Ujio wa Samsung Galaxy M22 wala haupo mbali

Ujio wa Samsung Galaxy M22 wala haupo mbali

Spread the love

Samsung wanaonekana kutumia njia mbalimbali kuwaambia watu kuhusu ujio wa simu janja kutoka kwao na safari hii imeonekana Galaxy M22 kwenye tovuti za kampuni nchini Malaysia na Singapore.

Wafuatiliaji wa masuala ya simu janja wameweza kuona Samsung Galaxy M22 kwenye tovuti za kampuni (Samsung) nchi mbili tofauti; Singapore na Malaysia huku rununu hiyo ikiwa bado haijazinduliwa. Hii maana yake nini? Kwa lugha rahisi Samsung wanatuambia tujitayarishe kumpokea mgeni mwingine kwenye soko la ushindani.

SOMA PIA  Ulinzi kwenye Windows 7 kusitishwa

Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa ikihusisha ujio wa Samsung Galaxy M22 lakini kwa kile ambacho kimeweza kuonekana kwenye tovuti za kampuni ndni ya nchi mbili tofauti rununu hii inaaminika kufananana kwa karibu sana na Galaxy A22 4G hivyo kuaminika kuwa na sifa hizi:

Kioo cha ubora wa Super AMOLED chenye urefu inchi 6.4, ung’avu wa kile kinachoonekana kwenye uso wa juu ni wa hali ya juu ukibebwa na 90Hz. Kamera zake zina MP 48, 8 na mbili MP 2 nyuma. Ile ya mbele inaaminika kuwa na MP 13.

Galaxy M22

Simu hii inatazamiwa kuja angalau katika rangi tatu tofauti na programu endeshi ya kwenye simu hii ni Android 11.

Sifa nyinginezo ambazo inaaminika kuwa simu janja husika inazo ni pamoja na kipuri mama kuwa Helio G80 SoC, RAM GB 4, 128 GB a diski uhifadhi huku ikiwa na sehemu ya kuweka memori ya ziada. Betri la kwenye simu hii linaaminika kuwa na 6000mAh, 25W za teknolojia ya kuchaji haraka halikadhalika kichwa cha chaji kuwa na uwezo wa kutoa 15W kwenda kwenye simu.

Galaxy M22

Simu hii huenda ikawa inagharimu $283.69 ambazo ni zaidi ya Tsh. 652,487 bei ya ughaibuni.

Hakika kuna mengi mazuri yatakayokuja katika siku za usonihivyo basi ni vyema ukaendelea kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania