fbpx

Mwaka 2017 teknokona tumeulizwa maswali 2,980

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mwaka 2017 kupitia ukurasa wetu wa Facebook tumewasiliana na wasomaji 745 pamoja na kuulizwa maswali zaidi ya 2,980 kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu teknolojia.

Kwa wastani kila siku tuliulizwa maswali manne yanayohusu teknolojia. Maswali mengi tuliyoulizwa kwa mwaka 2017 asilimia 95 yalihusu simu janja, 4% yalihusu masuala yanayohusiana na kompyuta na asilimia iliyobaki yalikuwa ni mengineyo. Maswali mengi pia yalijitokeza katika makala mbalimbali au taarifa tulizozichapisha katika tovuti yetu hii hayo hatukuyaingiza katika taarifa hii japo yalipatiwa majibu mazuri.

Mengi ya maswali kuhusu simu janja ilikuwa ni kutatua matatizo yaliyozikumba simu zao ikiwemo kuondoa lock ya FRP, kusahau nywila (password) kuhitaji kuweka programu kadhaa katika simu zao.

Maswali mengi yalikuwa ni kuhusu programu wezeshi (software) kwenye simu na yale ya hardware yalikuwa machache sana.

Asilimia 98 ya maswali tuliyoulizwa kuhusu simu janja ilikuwa ni zile za mfumo endeshi wa Android na asilimia 1.9 ilikuwa ni mfumo endeshi wa iOS na asilimia 0.1 ilikuwa mfumo wa Windows. Simu janja ambazo zimekuwa zikitajwa kutumiwa zaidi na wasomaji wetu ni Tecno (70%), Samsung (15%), Huawei (5%), na asilimia iliyobaki ni kwa simu nyinginezo.

maswali

VIfaa vya kidijiti vimekuwa msaada mkubwa kwa watu mbalimbali na hivyo maswali mengi yamekuwa yakitokana na vitu hivyo.

Aidha jambo lingine watu wengi waliohitaji ni kuelekezwa kuona mawasiliano ya mtu mwingine (Mke/Mpenzi). Hakuna yeyote aliyeelekezwa isipokuwa kukumbushwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Kumbuka Teknokona tupo kwa ajili ya kuelekeza, kujulisha na kufahamisha kile ambacho kina maslahi kwa jamii na kinachokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi. Kudukua mawasiliano ya mtu mwingine bila ya ridhaa yake ni kosa la kisheria kufanya hivyo. Bahati nzuri nchi zote duniani kufanya hivyo ni kosa la kisheria lenye adhabu kali.

INAYOHUSIANA  Huawei watoa MediaPad M5 lite

Pia wachache sana waliwasiliana nasi kwa ajili ya kutushauri na wengine kusalimia tu. katika kujibu maswali kuna ambao tuliwajibu haraka sana na wengine tulichelewa sana.

Kuchelewa inatokana na changamoto ya kulifanyia utafiti swali tuliloulizwa ili kupata jibu lenye uhakika na sahihi. Kwa wale ambao hawajajibiwa waendelee kuwa wavumilivu tutawajibu kwa maswali yao kwani yanahitaji utafiti kabla ya kujibiwa.

Baadhi ya maswali ya wasomaji wetu yalitufanya kuandaa makala kadhaa ili kusaidia wengi na kuepuka kurudiwa swali la aina moja kwa watu wengi.

Tunawaahidi wasomaji wetu kuendelea kuwafahamisha yote yanayojiri katika masuala ya teknolojia duniani kote. Tunashukuru sana wa ushirikiano wenu na kutuunga mkono.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.