Biashara yoyote ile inahitaji mtu kuwa mbunifu ili kuweza kufanikiwa kwa kuvutia wateja na pengine hata kutanua wigo wa kipato kinachopatikana. Samsung wamefikiria na kuamua kuja na Galaxy A21 ya kawaida tuu.
Samsung imefanya uzinduzi wa aimu janja huko Japan ambapo inalenga watu wa hali ya kati kutokana na kwamba rununu yenyewe haina vitu vya kutisha na kwa lugha rahisi ni “Ya kawaida tuu”. Katika miaka ya karibuni ni nadra sana kukutana simu janja ya Samsung ina kamera moja upande wa nyuma, sasa tuanzie hapo kwanza mengineyo ni kama ifuatavyo:
Kipuri mama|Kioo
Kwenye upande wa kipuri mama simu hii imewekwa Exynos 7884B SoC; uwezo wake ni wa kawaida kabisa lakini kinafaa kwa kwa ufanisi wa rununu husika. Urefu wa kioo ni inchi 5.8 ambacho muonekano wa vitu/mchanganyiko wa rangi ni wa hali ya juu bila kusahau sehemu iliyoingia ndani kidogo kwenye kamera ya mbele.
Kamera|Memori
Kwa upande wa memori ina RAM ya GB 3, diski uhifadhi ni GB 64 lakini ina sehemu ya kuweka mwemori ya ziada mpaka TB 1. Kwenye kamera nyuma ndio ipo moja tu ambayo ina MP 13+taa ya kuongeza mwangaza sehemu hafifu. Kamera ya mbele ina MP 5 pekee.

Uwezo wa betri|Mengineyo
Betri lake ni lile ambalo si la kuchomoa na kuchomeka, lina 3600mAh na hakuna taarifa kama rununu husika ina teknolojia ya kuchaji haraka. Inatunia USB-C, Bluetooth toleo la 5, WiFi, 4G LTE.

Simu hii itaingia sojoni mnamo Septemba 9 ya mwaka huu na itaanza kuuzwa huko Japan. Neno letu kuhusu simu hii ni kwamba inawafaa sana watu ambao hawana matumizi makubwa sana na rununu kuanzia kucheza magemu mazito mpaka kupiga picha zenye ubora wa juu sana.
Vyanzo: Gadgets 360, Gizmochina
2 Comments