fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kompyuta Teknolojia Windows 11

Wanaotumia kompyuta za zamani hawatazuiwa kuweka Windows 11

Wanaotumia kompyuta za zamani hawatazuiwa kuweka Windows 11

Spread the love

Watu wengi tuu duniani wameonekana kuwa na nia ya kutaka kutumia Windows 11 wakati sahihi utakapofika kwa maana ya kuzinduliwa rasmi na Microsoft. Katika kufanya mambo yavutie Microsoft imesema haizuia kompyuta za zamani kuiweka programu hiyo endeshi.

Nina amini wale ambao tunatumia kompyuta ambazo ni toleo la nyuma tuna wasiwasi kama kompyuta zetu zipo kwenye orodha ya zile ambazo zinaweza kuweka Windows 11. Microsoft wameliona hilo na kuamua mambo wazi kwamba hata wale ambao kompyuta zetu ni za zamani bado tunaweza tukaishusha na kuiweka kwenye vifaa vyetu.

SOMA PIA  Kongamano Kubwa la Masuala ya Teknolojia Kufanyika Jijini

Windows 11 kutobagua kompyuta

Kwa taarifa iliyopo kwa kompyuta zote ambazo Microsoft inaona zinafaa kuhamia Windows 11 zitapokea taarifa fupi ya kumjulisha mtumiaji kuwa anaweza kuishusha na kuiweka kwenye kifaa chake katika mtindo wa kupakua masasisho. Hata hivyo, wale ambao tuna kompyuta toleo la nyuma tunaweza tusipate hiyo taarifa fupi lakini mtu mwenyewe anaweza kuingia mtandaoni na kuishusha kisha kuiweka kwenye komyuta.

kompyuta za zamani

Windows 11 kuwweza kuwekwa hata kwenye kompyuta za zamani: Awali Microsoft walisema toleo hilo la programu litakuwa ni mahususi kwa kompyuta kuanzia kizazi cha nane au zaidi cha vipuri mama.

Lakini nguli hao kwwenye masuala ya kompyuta wamebadilisha mawazo na kueleza kuwa toleo hilo litakuwa kwa kompyuta hata zile za zamani kwa lengo la kupata maoni kuhusiana na programu hiyo endeshi.

SOMA PIA  Bidhaa za Apple zitakazotoka Septemba-Oktoba 2020

Ingawa kwamba toleo hilo la programu endeshi litapatikana katika kompyuta nyingi zaidi lakini ujue kuwa utaishusha huku bila kujua iwapo itaendana na viwezeshi (drivers) au vingninevyo ndani kompyuta yako na kama haziendani itakuwa ni hasara kwako kwani itakulazimu uitoe.

Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania