fbpx

Huawei kuachana na soko la Marekani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Taarifa zinasema kwamba Kampuni ya Huawei itasitisha kupeleka bidhaa zake katika soko la Marekani kutokana na vikwazo vingi inavyopata katika nchi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei, Xu Zhijun alisema waziwazi kuwa mambo mengine hayawezi kubadilishwa na wao Huawei na hawataendelea kulazimisha na kutumia nguvu kubwa katika soko ambalo wanaonekana hawahitajiki.

Huawei itaendelea kuzalisha bidhaa bora na kukidhi mahitaji ya wateja wao na kutengeneza na kuaminika zaidi sokoni.

Kampuni ya Huawei kwa muda mrefu imejaribu kupenya katika soko la Marekani lakini serikali ya nchi hiyo mara kwa mara imekuwa ikirudisha nyuma juhudi za kampuni hiyo.

Soko la Marekani

SImu Ya Huawei Enjoy 7 Plus — Toleo La KFC ambayo makao yake makuu yapo Marekani.

Katika taarifa yake ya maendeleo ya soko la Marekani Huawei imeonyesha hakuna ufanisi wowote wa mafanikio zaidi ya kushuka siku hadi siku na hivyo kuonekana kwa Kampuni hiyo kuondoka rasmi katika soko hilo.

INAYOHUSIANA  Huawei P30: Hizi hapa simu mbili mpya za Huawei za P30 na P30 Pro

Mwezi Februari mwaka 2018, wakuu sita wa ngazi za juu wa mashirika ya kipelelezi ya Marekani waliwaagiza wananchi wa Marekani kutotumia simu na vifaa kutoka kampuni ya Huawei. Kujua zaidi kuhusiana na taarifa hiyo BOFYA HAPA.

Inaelezwa kwamba kufikia mwishoni mwa mwaka huu Huawei inaweza kutoka kabisa katika soko la nchi ya Marekani na hii inadhirika baada kuachishwa kazi kwa wafanyakazi watano akiwemo Mkurugenzi wa Masoko ya Huawei kwa Marekani.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.