fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Masasisho kwenye simu janja za Samsung Galaxy S20

Masasisho kwenye simu janja za Samsung Galaxy S20

Spread the love

Samsung wameanza mwezi Septemba na masasisho ya kuzifanya simu janja zao mbalimbali ziwe salama ambapo mwezi huu rununu kutoka familia ya Galaxy S20 imepokea vitu vyake.

Kwa watu wenye Samsung Galaxy S20 na nduguze wa familia moja wafahamu ya kuwa masasisho kwa ajili ya kuifanya rununu kuwa salama zaidi kwa maana ya kwamba kuboresha/kuondoa madhaifu yaliyobainika kwenye simu hizo mwezi uliopita yamesharuhusiwa na yapo tayari kupakuliwa.

SOMA PIA  Jinsi ya Kuiwezesha Kompyuta Kujizima Yenyewe Usiku

Samsung Galaxy S20, S20, S20 FE+ na S20 Ultra ni simu janja ambazo zina wateja wengi lakini pia zikiwa ni rununu zinazovutia na tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2020 zimekuwa miongoni mwa vivutio vya watu wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Samsung Galaxy S20

Masasisho ya usalama kwa mwezi Septemba yafika kwenye simu janja za familia ya Galaxy S20.

Je, unafahamu kuangalia iwapo kuna masasisho yanayohusiana na programu enedeshi kwenye simu janja za Android?

Si kwa simu janja za Samsung tu bali hata nyinginezo inatupasa kufahamu jinsi gani ya kuangalia iwapo kuna masasisho au la! Basi ingia Settings>>Software Update kuweza kujua iwapo yapo au rununu husika bado haijapelekewa zawadi hiyo ya kila mwezi.

SOMA PIA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Daima ni muhimu kupakua masasisho kwa usalama na ufanisi wa vifaa vyetu vya kiganjani kwani kuma mengi ambayo yanaboreshwa kwenye simu janja na ni muhimu kuyashusha kwenye rununu zetu.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania