fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google Pixels simu Teknolojia

Masasisho ya mwezi Septemba kwa simu janja-Google Pixel

Masasisho ya mwezi Septemba kwa simu janja-Google Pixel

Spread the love

Masasiaho ya kila mwezi kwa simu janja-Google Pixel yameendelea kufikia simu hizo na kimsingi ndio zinazoiweka Google kwenye ramani ya ushundani kwa simu simu janja sokoni.

Masasisho kwenye simu janja yoyote ile ni kitu muhimu sana kwani yanakuja yakiwa na maboresho mbalimbali kuhusiana na toleo fulani la rununu. Katika hilo Google imekuwa ni kama desturi yao kupeleka masasisho kwenye simu janja za Google Pixel kila Jumatatu ya mwezi lakini mwezi huu jana ilikuwa ni “Siku ya wafanyakazi” nchini Marekani hivyo kwa heshima hiyo suala hilo halikufanyika hadi leo, Jumanne.

mwezi Septemba

Masasisho hiyo ni mahususi ya kwa ajili ya ulinzi kwa mwezi huu (Septemba).

Masasisho yenye namba RQ3A.210905.001 ambayo ni kwa wenye Pixel 3, 3 XL, 3a, 3a XL, 4, 4 XL, 4a, 4a (5G), na 5 ulimwenguni kote. Masasisho yenye namba RD2A.210905.002 ni mahususi kwa watumiaji wa Pixel 5a wa Amerika Kaskazini huku RD2A.210905.003 inawahusu wenye Pixel 5a nchini Japan.

mwezi Septemba

Simu janja za Google Pixel 5 na 5a zapokea masasisho ya mwezi Septemba.

Kama wewe unatumia Google Pixel zilizoorodheshwa hapo juu basi kumbuka kupakua masasisho hayo ya mwezi Septemba lakini bila kudhau kuwa na kifurushi cha kutosha kinachozidi ukubwa wa kile kinachotakiwa kushushwa halikadhalika nafasi ya kutosha iwepo kwenye simu.

Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania