fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Ifahamu vyema simu janja Samsung Galaxy A52s 5G

Ifahamu vyema simu janja Samsung Galaxy A52s 5G

Spread the love

Simu janja za Samsung  zimeendelea kuongezeka ambapo takribani wiki mbili zilizopita Galaxy A52s 5G ilizinduliwa ikiwa tayari kwa wale wanaopenda kupata raha ya 5G.

Simu janja ambazo zinatumia 5G zimeendelea kuongezeka ambapo Samsung wameonekana kuendelea kutoa rununu ambazo zinatumia teknolojia hiyo ya kisasa zaidi lakini pia yenye kasi. Samsung Galaxy A52s 5G ina mengi ya kuielezea ambayo yanaifanya simu hiyo ivutie. Sifa zake ni hizi:

Muonekano|Kioo

Hii ni rununu ambayo si pana (unene wake ni 8mm) na wala yenye uzito unaoudhi. Urefu wa kioo chake ni inchi 6.5 (1080*2400px, 120Hz), kioo chake ni cha ung’avu wa hali ya juu (Super AMOLED) na kamera ya mbele imewekwa katikati; inagwa pande mbili za kioo cha mbele mbele iliyowekwa chini ya kioo lakini katika mtindo wa kufanya mbele kuwepo kwa shimo dogo; kamera ya mbele ina MP 32.

Galaxy A52s 5G

Simu hii ina uwezo wa kuingia kutoingia maji katika kina cha hadi mita 1 kwenda chini kwa muda wa dakika 30. Kamera zote (mbele/nyuma zina uwezo wa kuchukua picha jonefu katika ubora wa 4K na 1080px).

Kipuri mama|Memori

Kwenye teknolojia ndani ya simu janja husika Samsung wameamua kuweka Qualcomm Snapdragon 778G 5G huku kwenye kipengele cha memori simu hii ina GB 128/256-diski uhifadhi+uwezo wa kuweka memori ya ziada. RAM ni GB 6 au 8.

SOMA PIA  Apps mbalimbali katika simu moja kwa akaunti mbilimbili

Betri|Kamera

Kivutio cha wengi kwenye simu janja mbali na vitu vingine lakini ubora wa kamera, uwezo wa betri huwa vinachochea kwa namna yake kuifanya rununu iuzike kirahisi. Betri ya kwenye simu hii ina 4500mAh, 25W ya teknolojia kuchaji haraka, inatumia USB-C 2.0.

Galaxy A52s 5G

Kamera za nuyma zina MP 64, 12 na mbili zina MP 5+taa ya kuongeza mwanga sehemu hafifu.

Mengineyo

Simu hii ipo ambayo inatumia kadi mbili za simu na toleo jingine inatumia kadi moja tu ya simu, inalindwa na kioo cha Gorilla 5 upande wa mbele na nyuma ni plastiki, inatumia Android 11, teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa chini ya kioo, inapatikana katika rangi Nyeusi, Nyeupe, Zambarau.

Galaxy A52s 5G

Samsung Galaxy A52s 5G ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, WiFi, Bluetooth 5.0, uzito wake ni gramu 189.

Bei yake ni $493|zaidi ya Tsh. 1,133,900 (6/128GB), $513|zaidi ya Tsh. 1,179,900 (8/128GB) na $610|zaidi ya Tsh. 1,403,000 (8/256GB) bei ya ughaibuni na tayari imeshaingia sokoni tangu Septemba Mosi.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] Samsung wameanza mwezi Septemba na masasisho ya kuzifanya simu janja zao mbalimbali ziwe salama ambapo mwezi huu rununu kutoka familia ya Galaxy S20 imepokea vitu vyake. […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania