fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple IPhone MacOS Teknolojia

Septemba 14: Apple wathibitisha shughuli ya uzinduzi wa bidhaa zao

Septemba 14: Apple wathibitisha shughuli ya uzinduzi wa bidhaa zao

Spread the love

Kwa wiki kadhaa zimekuwepo habari kuhusu uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za Apple mwezi huu lakini wahusika walikuwa hawajathibitisha hilo. Sasa ni rasmi Septemba 14 ndio tarehe ya shughuli yenyewe.

Zikiwa zimebaki siku kadhaa mpaka kufikia Septemba 14 ambapo dunia nitaweza kuona bidhaa mbalimbali ambazo Apple wamepanga kuzitambulisha kwa ulimwengu huku wengi wakitegemea kuona toleo linalokuja kwa upande wa simu janja nikimaanisha iPhone kuna vitu vingine ambavyo vitatambulishwa siku hiyo.

SOMA PIA  Uwezo wa 5G upo vipi? Fahamu yote muhimu kuhusu teknolojia ya 5G

Bidhaa za Apple zinazotegemewa kuzinduliwa Sept. 14

Tukio hilo litarekodiwa kwanza kisha kurushwa kwenye mitandao mbalimbali hivyo watu kuweza kuangalia kinachokuja ambapo mbali na iPhone 13 kuna vitu vingine vinategemewa kuzinduliwa. Vitu hivyo ni:

>Vipuri mama: Inaaminika kuwa tutaweza kuona iPhone 13 hasa toleo la “Pro” likiwa na maboresho makubwa kwenye muonekano wa vitu kwenye simu janja husika. Halikadhalika, inategemewa kuna maboresho kwenye kamera, vipuri mama vyenye kasi.

SOMA PIA  Simu ya Kwanza Inayotumia Ubuntu Yaingia Sokoni

>Saa janja: Toleo jipya la saa janja ni moja ya bidhaa zinazotazamiwa kuzinduliwa hasa ukizingatia Apple Watch 6 ilitoka mwezi kama huu mwaka jana.

Programu endeshi: Imezoeleka kuona Apple wakitoa tarehe ya ujio wa toleo mbalimbali za programu endeshi za kwao- iOS 15, iPadOS 15, watchOS 8, na macOS Monterey. Hapa pengine tukaona pia kompyuta mbalimbali za Mac hasa ukizingatia kipuri mama toleo jipya-M1 lipo karibu kuzinduliwa ingawa mwezi Septemba huwa ni mahususi kwa iPhone na Apple Watch.

Septemba 14

Sept. 14: Tukio la unzinduzi wa bidhaa kwa mwaka huu linaitwa “California Streaming“.

Shughuli nzima itarushwa kwenye tovuti ya Apple ambayo inaweza kufikiwa kupitia vivinjari. Pia, tukio hilo litaonyeshwa kwenye Apple TV. Haya sasa kama utapenda kuangalia uzinduzi huo basi ujiandae kuwa na kifurushi cha intaneti cha kutosha.

VyanzO: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania