fbpx
apps, Teknolojia, Twitter

RASMI: Amua nani awe na uwezo wa kujibu machapisho yako kwenye Twitter

rasmi-amua-nani-awe-na-uwezo-wa-kujibu-machapisho-yako-kwenye-twitter
Sambaza

Moja ya mtandao wa kijamii ambao hauna mambo mengi ni Twitter na pengine wengi kutoupenda/kuutumia mara kwa mara kutokana kutovutia kwa vile ambavyo wanapendezwa navyo. Sasa hivi kuna hii ya kuweza kuamua nani awe na uwezo wa kujibu machapisho yako.

Mwezi Mei mwaka huu Twitter ilipeleka kipengele hicho katika hatua ya majaribio ambapo badhi ya watu walipata uwezo wa kuchagua nani awe na uwezo wa kushiriki kujibu kile ambacho kimechapishwa na mhusika.

INAYOHUSIANA  Google yaongezwa kwenye SwiftKey

Kama usipofanya chochote basi yeyote yule ambae ataona chapisho lako atakuwa na uwezo wa kutoa maoni yake lakini ukiamua kufanya mabadiliko utaweza kuamua iwapo watu uliowataja kwenye chapisho tu ndio waweze kujibu ama wanaokufuata kwenye Twitter waandike yao chini ya kile ambacho utakuwa umekiweka.

kujibu machapisho
Twitter warasimisha uwezo wa mtu kuamua nani awe anajibu machapisho aliyoyaweka.

Inaweza ikawa ni jambo jema au baya kwa wale wapenzi wa Twitter lakini pia hii inatosha kuwa huzuni kwa baadhi ya watu kwani sasa mhusika anaweza akatenganisha wale ambao wanaandika mazuri na kutoruhusu kabisa anaowafahamu kutopata mrejesho mzuri kutoka kwao.

Utajuaje iwapo umezuiliwa kujibu chapisho la mhusika? Iwapo utaona alama ya Dunia hapo maana yake kila mtu anaweza akajibu, watu walio pamoja inamaanisha ni kwa wale tu wanamfuata mhusika ndio itawahusu lakini pia ukiona ishara ya “Kila mmoja” (@) hapo sasa inawahusu waliotajwa pekee kwenye chapisho husika ndio wanaweza wakasema ya kwao.

kujibu machapisho
Maelezo ya nani na nani wanaweza wakashiriki kujibu machapisho yako. Vilevile, yeyote yule anaweza akaona, akapenda na hata klichapisha tena kwa kunukuu (retweet).

Je, wewe umefurahiswa na suala hili la Twitter kukupa uwezo wa kupunguza watu wanaoweza kuandika maoni yao kwenye chapisho lako?

Vyanzo: Gadgets 360, The Indian Express

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|