Nothing Phone (1) ililiteka sana soko na kuacha wengi midomo wazi kwani ilikuja kivingine kabisa na sasa inategemewa kwamba mwaka 2023 itatoka Nothing Phone (2).
Kampuni ya Nothing ambalo linamilikiwa na mmoja kati ya waanzilishi wa OnePlus, Bwana Carl Pei ameweka wazi kwamba toleo hilo la Nothing Phone (2) la simu litatoka mwaka 2023
Nothing Phone (2) haitakua na mabadiliko makubwa sana katika swala zima la muonekano maana toleo hilo litajikita zaidi katika Software ambayo ni bora zaidi.
Ukiachana na hayo yote simu hii inategemewa kuwa na sifa za udani zifuatazo
12GB RAM huku ujazo uhifadhi ukiwa nia 256GB, betri 5,000mAh huku muonekano wa nje (jumba) halitakua na tofauti ukilinganisha na Nothing Phone (1).
Bwana Carl bado ameendelea kuweka wazi kwamba simu zote hizo mbili ni simu za hadhi ya juu kabisa japokua kama Nothing Phone (2) ikitoka itakua na hadhi ya juu zaidi.
Simu hii inatarajirwa kuzinduliwa rasmi katika nusu ya pili ya mwaka 2023, na mpaka sasa kampuni haijaweka mambo mengi wazi kuhusiana na ujio huo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani umeshawahi kutumia simu ya Nothing? Nini kimekuvutia zaidi katika kifaa hiki?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.