Elon Musk afanikiwa kuinunua Twitter, jambo ambalo limeendelea kuleta mazungumzo mengi mtandaoni ya kuunga mkono au kupingwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao huu maarufu.
Wiki chache nyuma tuliandika kuhusu Bwana Elon Musk kuweka ofa ya kununua mtandao wa kijamii maarufu wa Twitter, unaofahamika sana kama sehemu inayowapa watu wa kawaida, mashuhuri, makampuni na serikali kutoa taarifa, kufanya mazungumzo na ata midahalo.
Bwana Elon Musk anaona kwa sasa lengo lake la kuongeza uhuru wa kimaoni katika mtandao huu maarufu utafanikiwa. Musk tokea mwanzo alipoonesha nia yake amekuwa muwazi ya kwamba jambo lilisukuma uamuzi wake ni kutaka kuona hali ya uhuru na haki ya utoaji maoni inalindwa kupitia Twitter. Hivi karibuni mitandao mingi ya kijamii imejikuta ikichukua hatua kali dhidi ya maoni hasa yenye mlengo wa kisiasa wa upando wa kulia zaidi, na wengi wameona ni kama mitandao ya kijamii imekuwa ikijihusisha na unyimwaji wa sauti ya upande flani wa kisiasa.
Mwanzilishi wa Twitter, Bwana Jack Dorsey ameunga mkono manunuzi hayo. Kupitia akaunti yake ya Twitter Bwana Jack amesema ni uamuzi bora zaidi kwa Twitter na anaamini katika lengo na mageuzi yanayotaka kuletwa na Elon Musk.
Mambo muhimu ya kufahamu;
- Kwa kuinunua Twitter, kwa sasa Twitter itakuwa kampuni binafsi na itaondolewa kwenye soko la hisa
- Kuna uwezekano mkubwa Bwana Jack Dorsey akarudishwa kwenye usukani au akawekwa kwenye nafasi ya uongozi muhimu, Musk amesema muda mrefu ya kwamba bado atataka kushirikiana na baadhi ya watu
- Kuna hatihati mkurugenzi wa sasa, Bwana Parag Agrawal akapigwa chini
- Kuna baadhi ya vitu ambavyo tutegemee kuboreshwa zaidi – kutokana na mapendekezo ya Elon Musk. Anataka watu waweze kufanya marekebisho kwenye TWEETS iwapo wamekosea. Pia anataka suala la utambulisho wa akaunti rasmi ‘verification’ liwe la uwazi zaidi na lisilo la kibaguzi katika upatikanaji wake.
No Comment! Be the first one.