Mtandao mkubwa wa kijamii wa Twitter wa sasa inadhaniwa kwamba wamezima muuganiko wa kutumiwa na App za Third-party kwa makusudi kabisa.
Third-party Apps ni zile app ambazo zinatumiaa huduma fulani na kwa kawaida zinakua hazijazalishwa na watoaji wa huduma hio, kwa mfano utumia huduma ya Twitter bila ya kutumia App ya twitter (ile yao wenyewe).
Ni wazi kuwa kuna App kubwa sana ambazo unaweza kuzitumia ili kutumia huduma hiyo ya Twitter lakini kuanzia ijumaa App hizo zikawa zimeanza kuacha kufanya kazi.
Kikibwa kingine kilchotokea ni kwamba mpaka sasa kampuni ya Twitter imekaa kimya maana haijaweka wazi jambo lolote.
Pengine wengine wanafikiria kwa haraka haraka hii inaweza ikawa ndio sera mpya ya kampuni yaani kampuni kuanza kutoruhusu kutumika na App ambazo ni za nje.
Ukiachana na haya sasa kuna baadhi ya vyanzo vinasema kuwa kampuni hii ya Twitter imefanya jambo hili kwa makusudi kabisa. Lengo pia haliko wazi kabisa maana haifahamiki kama hapo ni ili kudhuru watangazaji au wazalishaji wa maudhui.
Vyanzo vingi pia vinasema kuwa taarifa za jambo hili zimevuja kwanza ndani kabisa ya kampuni hiyo na hii na mara baada tuu ya wafanya kazi wa kampuni hiyo kasambaza taarifa hizo baina yao na kisha kutoka nje
Je unadhani mtandao huu ni kwamba itakua imefanya jambo hili kwa dhamira kabisa ya kuondoa uhusiano na App hizo? Je kuna nini kingine kinakuja ndani ya mtandao huo
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.