Licha ya kuwa moja kati ya mtandao wa kijamii wenye mafanikio na nguvu kubwa bado mtandao wa Twitter hauchoki kuleta huduma mpya mabli mbali, sasa wanakuja na kitu kingine.
Twitter imekua ikija na vipengele vipya kadha wa kadha, ni siku chache nyuma tuu tulaindika kuhusiana na huduma yake mpya ya Co-Tweet.
Kwa sasa iko katika hatua ya majaribio kuja na huduma/kipengele kingine kinachokwenda kwa jina la Status.
Vyanzo vingi vinasema kipengele hichi ni cha zamani na kinawakumbusha kipengele kile cha mtandao wa kijamii wa MySpace.
Usishangae sana kuona bado tunaitaja MySpace, Haya turudi katika huduma hii ya Status kutoka Twitter, Hivi ni jinsi gani inavyofanya kazi?
I don't know how twitter managed to release a more embarrassing and unusable feature than cotweets in the same month but here it is. these are all the statuses you can use. no custom statuses allowed pic.twitter.com/2BPwku1qi1
— Takes Of Vesperia (@coolranchzaku) July 27, 2022
Hapa kitakachokua kinafanyika ni kwamba, kama mtu ukiwa unatuma tweet unaweza kabisa kuelezea namna unavyojisikia katika Tweet hiyo kwa kutumia Status.
Kwa haraka haraka ni lebo tuu za maneno ambazo zitakuwa zinatokea katika baadhi ya tweet ambazo watu watakua wanatuma katika mtandao huo.
Kingine cha kujua ni kwamba huduma hii kwa sasa inafanyiwa majaribio na baadhi ya kundi tuu, japokuwa mtandao haujaweka wazi ukubwa wa kundi hilo.
Lakini kama kawaida bado TeknoKona tunahisi huduma hii iko katika majaribio na pindi kampuni ikijiridhisha kuwa inafaa basi itaachia huduma hii kwa watumiaji wote wa Twitter.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje? Na wewe utapendelea kutumia hudumia hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.