fbpx
Intaneti, Tanzania, Teknolojia, Uchambuzi

Watanzania na mawasiliano kwa njia ya barua pepe

watanzania-na-mawasiliano-kwa-njia-ya-barua-pepe
Sambaza

Katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia zipo njia mbalimbali za kumuwezesha mtu kufanya mawasiliano kwa haraka na kupata jibu papo hapo au baada ya muda fulani, wengi wetu tunafahamu kuhusu barua pepe.

Kama mtaalamu wa TEHAMA lakini pia kwa jinsi dunia ya leo ilivyo matumizi ya barua pepe ni muhimu na rahisi huku wakati mwingine ikiwa mbadala wa kuweza kuwasiliana na watu kwa njia hiyo na niwe mkweli tuu nina muda mrefu sijatumia sanduku la Posta 😀 😀 😀 .

INAYOHUSIANA  Google kupigwa faini ya kuvunja rekodi barani Ulaya

Lakini kuna kitu kimoja ambacho kwangu mimi nakiona ni tatizo na si kwa mtu moja moja bali hata kwa taasisi, mashirika/makapuni mengi nchini Tanzania na shida yenyewe ni wahusika kutotilia maanani matumizi ya kidijiti katika kuwasiliana. Si mara moja, mbili au tatu nimeshawasiliana nao kwa njia ya maandishi kwenda kwa makampuni, serikalini, n.k bila ya kupata majibu mpaka ufuatilie kwa kwenda mpaka ofisini.

Tujiulize kidogo… Nini maana ya barua pepe?

Barua pepe ni teknolojia ya kufanya mawasiliano kwa njia ya maandishi ambayo inaunganishawa na intaneti kisha kupita kwenye kompyuta kubwa na baada ya hapo kwenda kwa inayemfikia. Kitendo hiki hufanyika kwa haraka sana na mara baada ya mlengwa kupokea ujumbe itambidi afungue kisha kuusoma halafu kukujibu/kutojibu.

kwa njia ya barua pepe
Huduma ya barua pepe inakuwa chini ya kampuni fulani ambayo ndio inamuwezesha mtu kufanya mawasiliano baada ya kujisajili na taarifa zake kuhifadhiwa.

Sasa ni mara nyingi tuu nimekuwa nikijiuliza kwanini Watanzania ni wazito kufanya mawasiliano kwa njia ya barua pepe ilihali mtu unakuwa umekabidhiwa eneo hilo la kujibu jumbe za watu? Ni kiburi tuu? Au kutokuwa na ujuzi wa kutumia kompyuta/simu vizuri? Je, ni kufanya kazi kwa mazoea kwamba atakuja tuu kufuatilia?

Mimi naamini mfumo huu wa kuwasiliana unarahisisha muda, faragha kwa wanaoutumia lakini pia msongamano wa wati kuja maofisini kupata taarifa ya kitu fulani wakati angeweza kumuandikia ujumbe na kupata majibu. Ni huduma inayolipiwa kila baaa ya muda fulani sasa kwanini tusiitumie vilivyo? Sina jibu ila jamani tubadilike!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|