Kama unapitia katika post za mtandao wa X ambao zamani ulikua unajulikana kama Twitter na unashangaa kuna post unaziona zinatokana na akaunti ambazo hujazifuata (follow) usishangae.
Sio kwamba kila mtu ambae anatumia X amekutana na hii adha maana imetokea kwa baadhi ya watu tuu.
Ni watu wengi lakini wametoa malalamiko yao ya kwamba wanapokea matangazo mengi ambayo hayana lebo ya kuonyesha kwamba hayo ni matangazo.
Ni kawaida kabisa katika mitandao ya kijamii kuona kabisa matangazo lakini matangazo hayo huwa yanakuwa na lebo ambayo imeandikwa ‘Sponsored’ na lebo hii iko mahususi kuonyesha watu kwamba hilo ni tangazo.
Mpaka sasa haijajulikana kwamba hili limetokea bahati mbaya au ni nini kimetokea lakini kwa harakaharaka ni kwamba kutakua tuu na tatizo limejitokeza kwani mtandao kama ule hauwezi fanya hili kwa makusudi.
WOW. It looks like X is no longer marking all paid posts as “ads.”
A follower sent me this screenshot, saying that they viewed this unmarked ad from @realsaltlake a “couple of times” on the Following tab. pic.twitter.com/heBTQokU4O
— Nandini Jammi (@nandoodles) September 6, 2023
Ni wazi kwamba bila kuwepo kwa lebo hiyo ni upotoshaji mkubwa kwa watumiaji wa mtandao husika na ni ukiukwaji mkubwa kwa sharia zinazoendesha mitandao hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani mtandao wa X utakua umefanya hivyo makusudi au ni bahati mbaya?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.