Disney Plus inaendelea kujiongezea wafuasi au kwa namna nyingine naweza kusema wateka katika huduma zake katika ulimwengu wa Ku’stream.
Pata picha miezi mitatu tuu ya mwanzo katika mwaka 2022 imejiongezea wateja milioni nane. Disney Plus mpaka sasa ina zaidi ya wateja mamilioni duniani kote.

Kitu kingine ambacho kinapelekea kamouni hiyo kuongezeka kwa wateja katika mtandao huo ni kuwa na kazi za filamu au michezo ya kuigiza ambayo inapatikana katika mtandao huo tuu.
Kumbuka hivi karibuni kumekua na filamu na michezo mingi kupitia mtandao huo kama vile MoonKnight , Cheaper by the Dozen na Encanto.
Ukiachana na hilo kwa upande wa Netflix bado hali si shawari kabisa maana imeripotiwa kuwa imepoteza zaidi ya wateja (Subscriber) laki 2.
Kupotea huko kwa wateja kwa Netflix ni kwa mara ya kwanz kabisa lakini mpaka sasa mtandao huo una wateja zaidi ya milioni 222.
HBO Plus na yenyewe imeonekana kujipatia wateja (Subscriber) wengi wapya. Hii inamaanisha kuwa kuna ushindani mkubwa katika soko hili.

Disney Plus kwa sasa ina zaidi ya wateja (Subscriber) milioni 137.7, na bado namba hii inakadiriwa kuzidi kupanda kutoka na kampuni hiyo kuwa na filamu na michezo ya kuigiza mingi ambayo inasubiriwa kwa hamu.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii Umeipokeaje? Na Je Ushawahi Kutumia Huduma Hizi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.