Nadhani habari za Elon Musk kuhusu kuinunua Twitter ushazipitia zote hapa na ile nyingine hapa, tumeshajua kashainunua sasa kama kawaida kuna maboresho/mabadiliko inabidi yatokee.
Ni wazi kuwa Bwana Elon anataka Twitter ni ya malipo ya awamu (subscription) kwa taasisi kubwa na haswa zile za kiserikali.
Aliweka hii wazi kwa kuandika katika ukurasa wake kuwa Twitter itakua bure kabisa kwa watumiaji wa kawaida, ila hawa wa serikali na makampuni/taasisi itabidi wachangie kiasi kidogo.
Twitter will always be free for casual users, but maybe a slight cost for commercial/government users
— Elon Musk (@elonmusk) May 3, 2022
Ngoja kwanza, hivi unaijua Twitter Blue.. Tulaindika kuhusu habari hiyo HAPA, haya tushajua ni huduma ya Twitter, lakini hii unalipia sio?
Wengi wanadhani kuwa bwana Musk anaweza tumia Twitter Blue ili kuliwezesha hili lakini kumbuka hata yeye mwenyewe alaikua akipinga baadhi ya vipengele katika Twitter Blue ikiwemo malipo yake ya dola za kimarekani 3 (ambayo aliona ni kubwa sana).
Mpaka sasa wengi wanasema sio mwenendo mzuri kwa mtandao huo kuanza kulipisha watu katika mtandao huo..kumbuka haya ni malipo mapya kabisa kwa watumiaji wengi (kundi hilo) wa mitandao ya kijamii.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la maoni, hili umelipokeaje?? Je kwa mawazo yako hili ni jambo jema?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.