Bilionea Elon Musk aitaki Twitter tena, aamua kuvunja mkataba wa manunuzi ya mtandao huo wa kijamii baada ya kushindwa kujiridhisha na idadi halisi ya watumiaji wake.
Ni kwa miezi kadhaa sasa ata kupitia akaunti yake ya Twitter Bwana Elon Musk alikua anasema ana wasiwasi na idadi ya watumiaji wa mtandao huo baada ya ripoti kadhaa kuonesha ya kwamba asilimia kubwa ya idadi ya watumiaji si watumiaji halisi. Bali ni ‘bots’. Bots ni akaunti ambazo haziendeshwi na watu halisi bali zinaendeshwa na programu za kompyuta.

Bots ni utumiwaji wa programu za kompyuta kuendesha akaunti ambazo zinaweza kuwa na lengo la kusambaza upotoshaji au zikawa ni bots za faida kwa jamii. Bots zenye faida ni zile ambazo zinatoa taarifa zenye umuhimu, mfano kuna bots zinazotuma taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa, utokeaje wa majanga n.k. Mfano kupitia YouTube kuna watu wanatoa huduma za kuongeza views za video kwa watu wanaolipa ili kupata views nyingi.
Twitter wanadai bots kwenye mtandao huo wa kijamii wanachangia asilimia 5 tuu ya watumiaji wote.
Musk alisema anaelewa na anakubali uwepo wa bots wenye faida kwenye mtandao wa Twitter. Anachopinga ni idadi ndogo ambayo uongozi wa Twitter unasema ni asilimia ya bots katika idadi ya watumiaji inayoweka kwenye ripoti zake.
Je jambo hili ndio limefikia mwisho?
Hapana, ingawa kwa uamuzi huu Musk anawalipa Twitter faini ya kuvunja makubaliano ya manunuzi bado uongozi wa Twitter umesema upo tayari kwenda mahakamani kulazimisha ukamilishaji wa ununuzi huo. Wanasema Elon Musk amechelewa kubadili uamuzi, na jambo hilo litakuwa na athari kwa kampuni. Kumbuka bodi ya Twitter ilikubali rasmi ofa ya Bwana Musk ya kununua kampuni hiyo Tarehe 25 mwezi Aprili mwaka huu.
Faini ya kuvunja mkataba ambayo Musk anailipa Twitter ni dola bilioni 1 (Takribani Trilioni 2.3). Ofa yake ya kuinunua Twitter ilikuwa ya dola bilioni 44 za Marekani.
Mwenyekiti wa bodi ya Twitter, Bwana Bret Taylor amesema kampuni hiyo italazimisha mauzo hayo kukamilishwa, kwa kwenda mahakamani.
Tutaendelea kufuatilia kwa karibu muendelezo wa sakata hili. Je unaona ni sawa Elon Musk kubadili uamuzi miezi miwili mbele?
Vyanzo: Sec.gov na vyanzo mbalimbali
No Comment! Be the first one.