fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple apps Google Intaneti Mtandao wa Kijamii simu Teknolojia

Urusi yadai kampuni kubwa za kiteknolojia kufungua ofisi zao nchini ifikapo 2022

Urusi yadai kampuni kubwa za kiteknolojia kufungua ofisi zao nchini ifikapo 2022
Spread the love

Urusi inazidi kutilia mkazo swala la makampuni ya kigeni ya kiteknolojia kufungua ofisi zao ndani ya mipaka yake. Miongoni mwa makampuni 13 yaliyotajwa na nchi ya Urusi kufungua ofisi zao huko ni pamoja na Meta, Twitter, TikTok, Apple, Telegram na Google.

Sheria za Urusi zinadai ofisi za ndani kwa “makampuni ya mtandao” yenye watumiaji zaidi ya 500,000 kila siku. Baadhi ya kampuni tayari zina ofisi na kwa wale wanaochukuliwa kukiuka sheria wanaweza kuwekewa vikwazo kamili au vizuizi vya matangazo yao, ukusanyaji wa data na uhamisho wa pesa.

kampuni kubwa za kiteknolojia

Picha: Baadhi ya makampuni makubwa ya kiteknolojia

Nchi ya Urusi inataka kutumia sheria kuwa na udhibiti zaidi juu ya kampuni hizo na maudhui yao. Pia Urusi imegombana na Apple mara nyingi, kwa mfano, ikiwa ni pamoja na faini kwa madai ya kutumia vibaya utawala wa Duka la Programu. Hatua hiyo pia inaweza kusaidia Urusi kushinikiza makampuni kudhibiti maudhui ambayo serikali inaona kuwa ya kuchukiza, kama vile machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanayounga mkono upinzani wa kisiasa kwa utawala wa Putin.

SOMA PIA  Samsung yawaomba watumiaji wa Galaxy Note 7 kuacha mara moja

Chanzo: YahooNews Engadget

Endelea kutembelea tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania