Ushirikiano kati ya Leica na Huawei ambao umedumu kwa miaka miaka kadhaa kati ya pande hizo mbili unaelekea kufikia tamati tayari kwa kuanzisha ushirikiano na kampuni nyingine.
Leica wamehusika kwenye kamera za Huawei P40, Mate 20 Pro, P20 Pro, P30 Pro (2019) wakisifika katika kufanya muonekano wa picha uwezo wa kuvutia kipekee lakini sasa ushirikiano huo unaelezwa unafikia tamati na tayari kampuni hiyo kutoka Ujerumani wanawafikiria kukaa chini na Xiaomi au Honor ama Sharp mojawapo kati ya hizo kuweza kufanya nayo kazi.
Nini sababu ya Leica kutaka kushirikiana na kampuni nyingine?
Haijafahamika kinagaubaga sababu iliyopo nyuma ya pazia iliyofanya Leica kufikiria kufanya kazi na makampuni mengine lakini wapo wanaoamini kuwa vikwazo vya kibiashara ambavyo Huawei imekuwa ikikumbana navyo vimechagiza wabia hao kuamua kuangalia fursa ya biashara mahali pengine.
Inaelezwa kwenye Huawei P50 ndio itakuwa simu janja ya mwisho kuona mkono wa Leica na tayari wabia hao wameshafanya mazungumzo na kampuni ambayo inatrazamia kufanya nao kazi.
Kamera za Leica kwenye Huawei P50 ndio zinatazamiwa kuwa za mwisho ishara yao ubia kati ya pande hizo mbili kufikia mwisho.
Wengi wanaweza wakahuzunishwa na taarifa hii ambayo ushirikano kati ya pande mbili tajwa ulianza kwenye toleo la P9 ila hakuna chenye mwanzo kisischo na mwisho. Sisi yetu ni macho kusubiri ubia mpya halikadhalika bidhaa murua sokoni yenye mikono miwili kufanikisha kitu kimoja.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.