HP Inc. ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya habari ya Marekani yenye makao makuu yake Palo Alto, California ambayo hutengeneza kompyuta mpakato (Laptop), kompyuta za mezani (Desktop), vichapishaji (Printer) na vifaa vinavyohusiana na hivyo pamoja na suluhu za uchapishaji za 3D.
Teknokona leo tunakuletea orodha ya matoleo mbalimbali ya kompyuta mpakato za mwaka 2021. Miongoni mwa matoleo hayo ni mwendelezo wa rununu za awali za HP Envy, HP Omen na HP EliteBook.
HP Envy 14 na Sifa zake: Kompyuta hii ina kioo chenye ukubwa wa inchi 14 na ubora wa pikseli 1920×1200, ina RAM GB16, Core i7 prosesa, inakuja na programu endeshi ya Windows 10. Nafasi yake ya kutunza mafaili ni T1 SSD bila kusahau kadi za picha za Nvidia GeForce GTX 1650 Ti. Pia kompyuta hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa masaa 16.

HP Envy 15 na Sifa zake: Kompyuta hii ina kioo chenye ukubwa wa inchi 15.60 na ubora wa pikseli 1920×1080, ina RAM GB12, Core i7 prosesa, inakuja na programu endeshi ya Windows 10. Nafasi yake ya kutunza mafaili ni GB256 SSD.

HP Omen 16 na Sifa zake: Kompyuta hii ina kioo chenye ukubwa wa inchi 16.10, ina RAM GB32 inakuja na programu endeshi ya Windows 10. Nafasi yake ya kutunza mafaili ni T1 SSD bila kusahau kadi za picha za Nvidia GeForce RTX 3070. Pia kompyuta hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa masaa 9.

HP Omen 17 na Sifa zake: Kompyuta hii ina kioo chenye ukubwa wa inchi 17.30 na ubora wa pikseli 1920×1080, ina RAM GB16, Core i7 prosesa, inakuja na programu endeshi ya Windows 10. Nafasi yake ya kutunza mafaili ni GB128 SSD bila kusahau kadi za picha za Nvidia GeForce GTX 1060.

No Comment! Be the first one.