fbpx

Sasisho muhimu kwa Huawei Mate 20 Pro

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ili kitu chochote kiendelee kuwa imara na kutoonekana kimezeeka/kuwa kuukuu ni muhimu sana kifanyiwe maboresho au matengenzo kila baada ya muda fulani kupita na ndivyo ilivyo tokea kwa Huawei Mate 20 Pro.

Watumiaji wa simu janja, Huawei Mate 20 Pro wamekuwa wakipata fedheha kutokana na kasoro fulani fulani upande wa kamera lakini hata teknolojia ya kutumia uso kama ulinzi.

Matatizo hayo ambayo kwa uchache sana yanajumuisha kushindikana kufunga kwa wakati fulani programu ya kamera, rangi kuwa sio nzuri sana wakati wa kutumia teknolojia ya rangi ya picha kulingana na mazingira; bila ya mtumiaji kuchagua (Master AI) lakini pia makosa madogo madogo upande wa ulinzi yaliyobanika mwezi Desemba 2018.

Huawei Mate 20 Pro

Sasisho muhimu kwa simu husika lililolenga kuboresha matumizi ya kamera na teknolojia ya kutumia uso na mchakato mzima wa kuishusha kwenye rununu utachukua MB 482.

Ni lazima kabla hujafikiria kupakua sasisho hilo kwenye simu, Huawei Mate 20 Pro Basi uwe na kifurushi cha intaneti kuanzia MB 500 lakini pia rununu iwe na chaji angalau 50% na kuendelea.

Vyanzo: GSMArena, 9to5Google

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Undani wa Moto Z4 kwa uchache
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.