fbpx
simu, Uchambuzi

Motorola One Fusion+, Ifahamu Simu mpya ya Motorola. #Uchambuzi

motorola-one-fusion-simu-mpya-uchambuzi

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Motorola One Fusion+ ni simu kutoka Motorola – hivi ni sahihi kusema hivi? Hapana, tunatakiwa kusema ni simu mpya kutoka Lenovo.

Soma historia nzima ya jinsi Lenovo walinunua biashara ya simu ya Motorola kutoka kwa Google

motorola one fusion+

Simu ya Motorola One Fusion+ imeshaanza kupatikana katika mataifa kadhaa ikiwa ni pamoja na yale ya bara la Ulaya na nchini India.

INAYOHUSIANA  PowerAmp 3.0 : App bora ya kusikilizia mziki yazidi kung'aa

Inakuja kwenye rangi nyeupe (Moonlight White) na ya blu flani hivi (Twilight Blue).

Motorola One Fusion+
Motorola One Fusion+

Sifa zake:

  • Snapdragon 730G SoC
  • RAM ya GB 6 na diski uhifadhi ya GB 128
  • Kamera nne kwa nyuma – Kuu ya Megapixel 64, ya picha pana ya megapixel 8 (ultrawide – nyuzi 118)
  • Kwenye kamera ya selfie ni ya Megapixel 16 na ni kamera ambayo inachomoka kutoka eneo la juu la simu pale unapoihitaji. Muda ambao haitumiki basi haionekani. motorola fusion one+
  • Betri ni la mAh 5,000 na inakuja na mfumo wa kuchaji wa USB C.
  • Teknolojia ya kufunga na kufungua kwa kutumia alama za vidole (fingerprint).
  • Teknolojia ya 4G, uwezo wa hadi laini mbili.
INAYOHUSIANA  Nokia kuja na simu yenye kicharazio cha QWERTY

 

Mengine: Inasehemu ya kutumia MicroSD na inaweza kusoma ya hadi TB 1, pia kuna Bluetooth v5, Wi-Fi 802.11 ac, GPS, & 3.5mm audio jack.

Ikianza kupatiakana nchini basi tegemea kulipa kati ya Tsh 800,000/= hadi 900,000/=. Bei yake kwa India na Ulaya haizidi Tsh 800,000 za kitanzania.

Je unaionaje simu hii? Je unadhani itatoboa sokoni ikiingia Tanzania?

 

Vyanzo: GSMArena na Motorola

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |