Mwaka umeguka na tumeshaanza mwaka mwingine makampuni mbalimbali yapo mbioni kutoa bidhaa mpya ambapo siku si nyingi utasikia kuhusu simu mpya za BlackBerry na Alcatel.
TCL Corporation ndio wamiliki wa sasa bidhaa zinazobeba jina la BlackBerry na Alcatel na katika onyesho la Consumer Electronics Show (CES) 2019 watazindua bidhaa zao mbalimbali zikiwemo teknolojia ya kwao kwenye upande wa vioo; zilizo na kona pembezoni mwa kioo na zenye nukta ndogo katikati upande wa kamera.

Blackberry je?
Blackberry wenyewe hawategemei kutoa simu mpya sipokuwa kutambulisha ubia wao na makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano hasa kwa simu zao za karibuni; BlackBery Key 2 na Key 2 LE wakilenga zaidi soko la Marekani na nchi nyingine duniani.
Onyesho la CES 2019 linatazamiwa kufanyika wiki kesho huko Las Vegas, Marekani ambapo makampuni mbalimbali yatashiriki kuonyesha vitu vipya kutoka kwao.
Vyanzo: Android Authority, GSMArena