Katika dunia ya leo ambapo teknolojia imetawala sio lazima kusubiri mpaka bidhaa husika itoke ndio uweze kujua sifa zake bali muda inavyozidi kusogea unaweza kufahamu kitu kimoja mpaka kingine.
Simu janja, Samsung Galaxy S10 Lite bado haijatoka kabisa lakini tayari kutokana na chazo cha kuaminika imeshabainika uwezo ambao betri ya simu husika itakuwa nayo lakini hata aina ya kipuri ambacho kitawekwa kwenye rununu hiyo.
Betri.
Samsung Galaxy S10 Lite inaelezwa kuwa na betri ya nguvu kiasi cha 3100mAh kwa mujibu wa taarifa na picha iliyoonekana kwenye vyanzo mbalimbali vya taarifa ulimwenguni.
Kipuri mama.
Watu wengi tunaposikia toleo la simu likiwa ninamalizia na neno “Lite” basi moja kwa moja tunajua uwezo wake utakuwa ni wa chini kidogo kulinganisha na mtangulizi wake, si ndio?. Mambo ni tofauti kwa Samsung Galaxy S10 Lite ambayo inaelezwa kuwa naΒ Snapdragon 855 au Exynos 9820 hizo zikiwa ni moja ya vipuri mama vyenge nguvu kabisa na karibu mara zote huwa zinawekwa kwenye toleo la kwanza kabisa kwa simu husika.
Simu hii, Samsung Galaxy S10 Lite inategemewa kutoka ndani ya miezi michache ijayo ila kabla hatujapata kujua kila kitu tutakuwa tumeshapata dodoso mbalimbali kuhusiana na rununu husika.
Vyanzo: GSMArena, SoyaCincau