fbpx

Huawei, simu, Uchambuzi

Huawei P30: Hizi hapa simu mbili mpya za Huawei za P30 na P30 Pro

simu-huawei-za-p30-pro-uchambuzi

Sambaza

Kampuni ya utengenezaji wa simu ya Huawei Jumanne ya wiki hii ilizindua simu mbili za Huawei P30 na P30 Pro katika jiji la Paris nchini Ufaransa.

huawei p30
Kamera yake inayokuja na sensa ya Megapixel 40 ni moja ya kitu bora zaidi kwenye Huawei P30.

Simu ya P30 ni mfululizo wa simu za familia ya ‘P’ ambazo huwa za kiwango bora na cha juu hususani katika upande wa kamera.

Unakumbuka ubora wa P20 na P20 Pro zilivyokuwa na ubora mzuri kiasi cha kuitwa ‘wafalme wa kamera’?. Basi P30 inakujia na Kamera nne, tatu za nyuma na moja ya mbele (Selfie).

huawei P30

Kwa upande huu wa kamera Huawei wameonesha ushindani kwa wale wanaokuja na simu zenye kamera nzuri. Kamera ya P30 itakuwa na uwezo wa ku Zoom mara 30 mpaka 50, ambapo kwa kamera za simu nyingine bado kufikia uwezo huo.

SOMA PIA  Tecno waingia mkataba wa kimatangazo na timu ya Manchester City

Moja ya kipengele kingine kinachovutia kwa P30 ni kwamba ina alama ya IP53 kwa maana ya kuwa na teknolojia ya kuzuia vumbi na kuingia maji ndani ya simu hiyo pamoja na rangi ya kuvutia nyuma ya mfuniko wake.

huawei p30
Muonekano wake
  • Hata hivyo P30 zimeboreshwa zaidi na kwa kiwango kizuri kuliko P20 zilizotolewa mwaka jana.
  • Huawei P3 inakuja na kioo cha ukubwa inchi 6.1 kikitengenezwa kwa teknolojia ya OLED.
  • Kwa upande wa prosesa inakuja na aina ya HiSilicon kirin 980(7nm) ambapo ujazo wa betri ni 3,650mAh kwa P30 na ujazo wa 4000 kwa mAh.
SOMA PIA  Simu rununu Realme 2 Pro imetoka

Baadhi ya sifa za Huawei P30 na Huawei P30 Pro angali hapo chini kama ifuatavyo

           KIPENGELEHUAWEI P30HUAWEI P30 PRO
Ukubwa wa kioo6.1-inch OLED
19.5:9, FHD+
2340×1080 pixels
6.47-inch Curved OLED
19.5:9, FHD+
2340×1080 pixels
Mfumo wa AndroidAndroid 9 Pie
EMUI 9
Android 9 Pie
EMUI 9
Ujazo wa Betri3,650mAh4,200mAh
Kamera ya Nyuma 140MP SuperSpectrum
Wide angle, f/1.8
40MP SuperSpectrum
Wide angle, f/1.6, OIS
Kamera ya Nyuma 216MP Ultra wide angle, f/2.220MP ultra wide angle, f/2.2
Kamera ya Nyuma 38MP
3X Optical zoom, f/2.4, OIS
8MP Periscope
5X Optical zoom, f/3.4, OIS
Kamera ya Selfie
32MP, f/2.032MP, f/2.0
Uwezo wa Kamera KuZoom3X Optical Zoom
5X Hybrid zoom
30X digital zoom
5X Optical Zoom
10X Hybrid zoom
50X digital zoom
Diski uhifadhi/RAMRAM GB 6
Ujazo GB 128
RAM GB 8
GB 128GB / 256 / 512
SOMA PIA  Huawei na ZTE zapigwa marufuku

Kwa yeyote ambae angependa kumiliki simu hizo, kwa sasa dirisha lipo wazi kwa Pre-Order ambapo Huawei P30 inauzwa kwa Euro 680 takribani shilingi za kitanzania 1,782,000.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.