fbpx
Nokia, simu, Teknolojia

Toleo jipya la Nokia 5310 Xpress Music

tpleo-jipya-la-nokia-5310-xpress-music
Sambaza

Kwa yeyote ambae alipenda kusikiliza muziki kwenye simu miaka ya 2007 na kuendelea lazima atakuwa anaikumbuka Nokia 5310 Xpress Music.

HMD Global wameendelea kuwakumbusha watu zaidi ya muongo mmoja nyuma kwa kurudisha machoni pa watu simu ambayo iliwahi kupendwa na wengi kutokana na uwezo wake wa kutoa muziki kwa sauti ya juu. Sasa ni miaka kumi na mitatu baadae wameona inafaa kuirudisha sokoni Nokia 5310 Xpress Music ikiwa na maboresho mengi lakini bila kuacha asili yake.

INAYOHUSIANA  Toshiba Wakuletea Tableti ya Window 8.1 kwa Tsh Laki 2

Niwe muwazi tuu kwa kusema mimi ni mmoja kati ya watu wengi ambao simu hii nilitokea kuipenda kweli kwa sababu ya kile ambacho simu hiyo imewezeshwa; kutoa sauti ya muziki kwa sauti ya juu na kujiona kama upo kwenye ukumbi wa starehe ukifurahia muziki 😆 😆 😆 .

Rununu hii ina uwezo wa kawaida na kasi yake ya intaneti ni 2G lakini toleo jipya imeboreshwa umbo, kipuri mama ni MediaTek MT6260A SoC, kioo chake ni cha inchi 2.4, spika mbili (2) za mbele, sehemu za kuwekea kadi mbili za simu; mojawapo ikwa na uwezo wa kukubali umbo dogo kabisa kihifadhi namba za simu. kamera+kimulika cha kufanya picha kuwa ang’avu.

Vilevile, memori ya ndani ni 16MB lakini ina uwezo wa kukubali uhifadhi wa zidada mpaka GB 32, RAM MB 8. Betri yaina 1200mAh; inadumu na chaji kwa muda wa saa saba na nusu (iwapo mtu ataitumia kwakuongea na simu), siku 22 kama utaruhusu kadi zote mbili kuwa hewani na siku 30 iwapo utaacha kadi moja tu ndio ipatikane.

Nokia 5310 Xpress Music
Nokia 5310 Xpress Music: Simu iliyotokea kupendwa miaka ya 2007 kuendelea. Inapatikana kwa rangi Nyekundu/Nyeupe na Nyeusi/Nyekundu.

Tayari imeshazinduliwa na bei yake ni $~41.96|Tsh. 96,508 na inategewewa kuwa itaingia sokoni Mezi huu (Machi 2020). Vipi tuambie kurudi kwa simu umefurahishwa?

Vyanzo: Gadgeets 360, Slash Gear

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|