fbpx
Apple, Samsung, simu

Simu za 2019: Hizi ndio simu 10 zilizouzika zaidi mwaka 2019

simu-za-2019-hizi-ndio-simu-10-zilizouzika-zaidi-mwaka-2019
Sambaza

Je, katika simu za 2019 ulizozipenda kuna ambazo zinaweza zikawa kwenye orodha ya simu 10 zilizouzika zaidi kwa mwaka huo?

Hii ni orodha ya simu zilizofanya vizuri zaidi sokoni kwa mwaka 2019. Data hizi ni kulingana mauzo ya simu, na ni data zilizothibitisha na vyanzo mbalimbali. Kikubwa katika orodha hii ni kwamba Samsung na Apple wameingiza simu tisa kati ya kumi zilizo kwenye orodha hii. Ukiangalia utagundua pia kuna simu zilizotoka miaka ya nyuma ya 2019 lakini bado ziliuzika sana mwaka huo, mfano iPhone 8 ilitoka 2017

Namba moja: iPhone XR

simu za 2019 simu zilizouzika 2019
Simu za 2019: Katika orodha ya simu 10 zilizouzika zaidi duniani kwa mwaka 2019 ni chache sana ziliingia sokoni kabla ya mwaka huo.

Simu ya iPhone XR ndiyo simu iliyoshika namba moja katika orodha hiyo. Na imepita simu iliyoshika namba mbili, iPhone 11 kwa takribani asilimia 1 tuu.

INAYOHUSIANA  IPad Mini: 'Toleo la IPad Dogo na Bei Rahisi Lipo Njiani.'

Orodha nzima na simu zingine zilizoingia kwenye orodha ya simu 10 zilizouzika zaidi na kiasi zilivyoshika soko kimauzo kwa mwaka huo – kiasilimia.

Namba moja – Apple iPhone XR

Idadi ya iPhone XR zilizouzika ni asilimia 3 ya mauzo yote ya simu janja mwaka 2019.

Simu za 2019 iphone xr

Namba 2 – Apple iPhone 11

Asilimia 2.1

Apple iPhone 11 Simu za 2019

Namba 3 – Samsung Galaxy A50

Asilimia 1.8

Samsung Galaxy A50

Namba 4 – Samsung Galaxy A10

Asilimia 1.7

Samsung Galaxy A10

Namba 5 – OPPO A5 (2019)

Asilimia 1.3

Oppo A5

Namba 6 – Apple iPhone 8

Asilimia 1.2

Apple iPhone 8

Namba 7 – Samsung Galaxy A20

Asilimia 1.1

Samsung Galaxy A20

Namba 8 – Apple iPhone 11 Pro Max

Asilimia 1.1

iPhone 11 Pro Max

Namba 9 – Apple iPhone 7

INAYOHUSIANA  iPhone X yabainika kuwa na tatizo kwenye uwanja wa kuandikia sms

Asilimia 1.1

iphone 7 Simu za 2019

Namba 10 – Apple iPhone XS Max

Asilimia 1.0

iPhone XS Max Simu za 2019

Kama unavyoona nafasi 6 zimechukuliwa na Apple wakati Samsung wamechukua nafasi 3. Simu za hadhi ya kati kama vile Samsung Galaxy A20 na A50 zinaonekana kufanya vizuri zaidi kimauzo kwa Samsung kuliko h0ata simu zao za hadhi ya juu zinazoshindana moja kwa moja na simu za iPhone.

simu za 2019
Data zinaonesha pia kwa barani Africa na Mashariki ya Kati Samsung ndiye aliyechukua nafasi tano za juu

Data zinaonesha pia kwa barani Africa na Mashariki ya Kati Samsung ndiye aliyechukua nafasi tano za juu za mauzo ya simu ambapo simu za Samsung Galaxy A10, A2 Core, A50, A20 na A10s ndizo zilizouzika zaidi.

Kwa Marekani nafasi zote tano za juu zilichukuliwa na Apple kupitia iPhone XR, 11, 8, 11 Pro Max na XS Max. Kwa Ulaya Samsung ndio iliongeza, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Samsung Galaxy A50, nafasi ya pili na tatu zilienda kwa Apple kupitia iPhone XR na 11 wakati nafasi ya nne na tano zilirudi kwa Samsung kupitia Galaxy A10 na A40.

INAYOHUSIANA  Nokia 8 Sirocco: Simu janja matata, yenye kava imara

Data hizi zinaonesha bado Apple amelishikilia vizuri soko la simu za hadhi ya juu – hasa Marekani (moja ya soko kubwa la simu janja), ila pia inaweza ikaonekana suala hili linasababishwa na Samsung kuwa na simu nyingi sana ata kwa zile zenye uwezo wa juu wa kushindana na za Apple.

Je, ni simu gani katika orodha hii hukutegemea kuikuta?

Chanzo: Counterpoint & SlashGear
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |