fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung wazindua Galaxy A11 kimyakimya

samsung-wazindua-galaxy-a11-kimyakimya
Sambaza

Wakati mwingine si lazima shamrashamra ziwepo kuonyesha/kutangazia umma kitu fulani bali unaweza kutumia njia mbadala na kufanikisha jambo lako na hivyo ndivyo ilivyozinduliwa Samsung Galaxy A11; mambo yalienda kimyakimya.

Kwa wale wapenzi na wafuatiliaji wa simu janja za Samsung wanafahamu fika kuna matoleo tofauti tofauti ya rununu kutoka familia ya Galaxy A (A10, 10s, A20, n.k). Hivi karibuni kampuni hiyo yenye makao makuu yake Japan iliamua kuweka bidhaa hiyo mpya kwenye tovuti yao tu bila kuiandalia uzinduziambapo watu, wanahabari wangeweza kualikwa kushuhudia tukio hilo.

INAYOHUSIANA  Mwanasayansi agundua Viwavi jeshi wanaokula Plastiki na kuozesha ndani ya wiki

Simu hiyo ambayo inaelezwa kuwa ya uwezo wa kati ina sifa za kuvutia na pengine kuleta ushawishi hivyo basi kuongeza mapato kwa kampuni husika lakini hata ushindani kwa bidhaa nyinginezo. Samsung Galaxy ina sifa zifuatazo kama zilivyoainishwa kwenye jedwali lifuatalo:-

Kipengele

Uwezo

Kioo Inchi 6.4 LCD (720*1560px)
Kipuri mama+Kasi yake Octa-core 1.8 GHz
Kamera

Nyuma: Kuna kamera tatu-MP 13, MP 5 na MP 2 + LED flash

Mbele: MP 8 ya muundo wa duara dogo

Diski uhifadhi

RAM: GB 2 na GB 3

Memori ya ndani: GB 32 + 32GB ya uhifadhi wa ziada

Mengineyo

Ulinzi wa kutumia alama ya kidole umewekwa kwa nyuma, betri lina uwezo wa 4000mAh, inatumia kadi mbili (2) za simu, inapatikana kwa rangi Nyeusi, Nyekundu, Nyeupe, Bluu.

INAYOHUSIANA  Tigo kuwabadilishia simu wenye simu feki! #Ofa
Samsung Galaxy A11
Rangi mbalimbali za Samsung Galaxy A11.

Bado haijajulikana lini itaingia sokoni wala bei yake lakini haitakuwa ya ghali kutokana kuwa kwenye kundi la simu zenye ubora wa katikati.

Vyanzo: GSMArena, Tech Radar

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|