Olimpiki 2020 ni michezo ambayo Dunia nzima inafahamu kuwa itakayofanyika huko Tokyo-Japan hapo mwakani wakati wa majira ya joto. Kwa wadhamini mbalimbali michezo hiyo ni fursa kwao kwa kutoa bidhaa zitaobaki kuwa ukumbusho daima.
Makala hii haitagusia sifa za simu janja, Samsung Galaxy S10+ lakini kile ambacho kampuni husika imepanga kufanya wakati wa michezo hiyo ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili (2); Samsung imejipanga kutoa toleo maalum la simu husika ambalo litakuwa na nembo ya michezo hiyo itakayofanyika mwaka 2020 huko nchini Japan.
Hii sio mara ya kwanza au ya pili kwa Samsung kuweza kupata nafasi ya kudhamini michezo hiyo bali wamekuwa wakipata nafasi hiyo tangu mwaka 1998 mpango huo unaaminika utaendelea mpaka Olimpiki 2028.
Je, toleo hilo maalum litapatikana duniani kote?
Kwa mujibu wa taarifa za awali zinaeleza kuwa simu hiyo itaptikana nchini Japan pekee na zitaundwa Samsung Galaxy S10+ zipatazo elfu 10 zitakazoanza kutengenezwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu huku kila moja itauzwa wakati wa michezo hiyo kwa $1,000|zaidi ya Tsh. 2.3M.
Simu nyingine ambazo zimewahi kutoka kwa toleo maalum la Olimpiki ni  Galaxy Note 8 (2018), Galaxy S7 edge (2016), Galaxy Note 3 (2014), Galaxy Note (2012).
Vyanzo: GSMArema, 9to5Google
One Comment
Comments are closed.