Kuhifadhi picha ya wasifu ya yule ambae anatumia WhatsApp Imekuwa ni jambo la kawaida sana na hatimae kuweza na kuweza kuitunza kwenye simu yako lakini kwa mujibu wa masasisho ya karibuni kwenye programu tumishi husika kitu hicho hakiwezekani tena!.
Sio kitu cha ajabu kuperuzi huku na kule ukiangalia picha za wasifu (DP-Display Picture) na kwa wengine ile ambayo itakupendeza unachukua hatua ya kuitunza ili kuwa nayo kabla ya mhusika kubadilisha na kuweka nyingine. Sasa kitu hicho inaonekna kimeondolewa kwenye WhatsApp na WhatsApp Business kwa Android na iOS.
WhatsApp wameondoa kitu hicho upande mmoja tu, bado unaweza ukaitunza picha ya wasifu kutoka kwenye kundi lakini si ya mtu binfasi.

Hii inawezekana ikawa ni habari njema kwa watu lakini watumiaji wengine wa programu tumishi yenye idadi kubwa wanaoitumia (zaidi ya bn 1.5) wakawa wamehuzunisha na kitendo hichpo. Tuambie wewe msomaji wetu umeipokeaje habari hii?
Chanzo: BGR