fbpx
Samsung, simu, Uchambuzi

Samsung: Samsung Galaxy S10 ni familia ya simu nne! Fahamu vipya kutoka Samsung

simu-za-samsung-galaxy-s10-uchambuzi

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Samsung Galaxy S10. Ni miaka kumi tokea matoleo ya simu ya Samsung Galaxy S yaanze kutolewa, Samsung watambulisha toleo la kumi la Samsung Galaxy S na hawakutambulisha simu moja tuu.

Samsung wametambulisha simu ya Samsung Galaxy S10 inayokuja katika matoleo tofauti manne, na pia wametambulisha Samsung Galaxy Fold – simu yenye uwezo wa kukunjwa na kukunjuliwa na kuchukua ukubwa wa sifa ya tableti.

Familia ya toleo la simu za Galaxy S10 kuna Glaxy S10, Galaxy S10 Plus, Galaxy S10E na Galaxy S10 5G.

Samsung Galaxy S10
Samsung Galaxy S10 Plus kushoto, Samsung Galaxy S10 kulia.

Kuna teknolojia mbalimbali za kisasa zimehusishwa kwenye simu hizi kama vile mtokeo wa eneo la kamera ya selfi ambayo imezungukwa na display/kioo (Teknolojia iliyopewa jina la Infinity-O Display). Teknolojia ya kuondoa lock/kufungua simu kwa kuweka kidole juu ya display/kioo cha simu. Pia kuna hadi kamera nne nyuma. Diski uhifadhi wa hadi TB 1…..na pia kwenye toleo la Galaxy S10 5G ni teknolojia ya kisasa ya intaneti ya 5G ambayo bado ata mitandao mingi ya simu duniani haijaanza kuitumia.

UNLOCK Samsung Galaxy S10
Samsung Galaxy S10: Teknolojia ya kisasa zaidi ya ufunguaji wa simu /unlock.

> Galaxy S10 – Dola 900

Toleo mama, au la kuanzia la Galaxy S10 linakuja na display ya inchi 6.1, ambayo inakuja katika kiwango kikubwa cha HD – mfumo wa 4K, HDR10.

Nyuma ina kamera 3, ambapo moja ni ya megapixel 16 kwa ajili ya picha za upana mkubwa. Nyingine kuu ni ya megapixel 12 na nyingine ni ya megapixel 12 kwa ajili ya rangi na ina zoom 2x.

INAYOHUSIANA  Vidokezo vya iPhone XR 2019

Kwa ajili ya selfi unapata kamera ya megapixel 10, ikiwa na teknolojia ya ‘dual aperture’ – teknolojia hii uhakikisha kamera itaongeza mwanga zaidi kama itagundua unapiga picha katika eneo la giza.

 • Kuna toleo la diski ujazo wa GB 128 na la GB 512, matoleo yote yanakuja na RAM ya GB 8. Pia una uwezo wa kutumia memori kadi hadi ya GB 512.
 • Betri ni mAh 3,400
 • Umbo la display ni lile lilozoeleka kwa sasa la kupinda mwishoni – kushoto na kulia (curved). Pia inateknolojia ya Gorilla Glass 6 mbele na Gorilla Glass 5 nyuma.
 • Prosesa ya kisasa zaidi ya Snapdragon 855.
 • Teknolojia zingine: Teknolojia ya kuchaji bila waya na Wi-Fi toleo la 6.
 • Rangi: Toleo hil na S10 Plus na S10E yote yanakuja kwenye rangi za ‘Flamingo Pink’, Canary Yellow, Prism Green na Prism Blue, Prism Black na Prism Whote.

> Galaxy S10 Plus – Diski uhifadhi wa TB 1 kwa bei ya Dola 1000

Kwa zaidi ya Tsh 240,000 zaidi ya bei ya Galaxy S10, kuwa zaidi ya Tsh Milioni 2.3 unapata toleo la Galaxy S10 Plus.

Hii inakuja na display ya inchi 6.4, na betri kubwa zaidi la uwezo wa mAh 4,100.

Teknolojia ya kamera zipo sawa na za S10 ila kwenye selfi huku utapata kamera mbili. Ya kwanza ni sawa na ya Galaxy S10, yaani ya Megapixel 10, na nyingine ya pili ni ya megapixel 8 inayoboresha kiwango na ubora wa picha za selfi.

INAYOHUSIANA  iPhone 6, Samsung Galaxy S6 Au Htc One M9: Simu Ipi Rahisi Kutengeneza Ikiharibika?
samsung galaxy s10 plus
Kamera kwenye S10 Plus

Kuna toleo la S10 Plus la diski uhifadhi wa GB 128, GB 512 na pia kama unataka uhifadhi wa ajabu basi utaweza nunua toleo la TB 1 ya diski uhifadhi linalokuja na RAM ya GB 128.

Teknolojia zingine ni sawa na toleo la S10.

> Galaxy S10E: Toleo la bei ‘nafuu’

Toleo la Galaxy S10E ndilo linalochukuliwa kama toleo la bei nafuu, hili linaanza kwa dola 750, ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 1.7.

SAMSUNG GALAXY S10E
Toleo la S10, S10 Plus na mwishoni ni S10E

Hii inakuja na display ya inchi 5.8.

 • Tofauti nyingine kuu ni kwenye kamera, ambapo hapa kuna kamera mbili tuu nyuma – kamera ya lens za rangi zaidi (telephoto lens) imeondolewa. Pia kwenye selfi unapata kamera moja tuu ya megapixel 10 kama kwenye toleo la Galaxy S10
 • Teknolojia ya display iliyopinda kushoto na kulia (curved) pia haijatumika, na teknolojia ya kufungua/unlock kwa alama za vidole kwenye display/kioo cha simu haipo bali wameweka teknolojia ya kawaida ya kusoma alama za vidole. Hii imewekwa eneo la pembeni kwenye kidude cha kuzimia simu.
 • Kiwango cha betri nacho kimepunguzwa, hapa unapata betri la mAh 3,100.
 • Kuna toleo la diski ujazo wa GB 128 ikiwa na RAM ya GB 6 au toleo la GB 256 likija na RAM ya GB 8.
 • Teknolojia ya Gorilla Glass 5 imetumika kwenye display mbele na eneo la nyuma ya simu.
 • Kwenye prosesa bado nayo inatumia prosesa ya Snapdragon 855.
INAYOHUSIANA  Apple wameboresha/kuleta vitu vipya kwenye iOS 12

> Galaxy S10 5G: Bei bado haitangazwa.

Toleo hili ambalo kikubwa ni uwepo wa teknolojia ya kisasa ya huduma ya intaneti ya 5G litakuja na display ya inchi 6.7.

 • Kwenye eneo la kamera itakuja na kamera mbili kwa ajili ya selfie na kamera nne nyuma. Kamera ya nne ni ya uwezo wa teknolojia ya lenzi yenye uwezo mkubwa zaidi wa utambuzi – 3D depth sensing camera.
 • Betri la mAh 4,500
 • Diski uhifadhi wa GB 256 pamoja na RAM ya GB 8, hili ndio toleo pekee katika familia ya S10 linalokuja bila uwezo wa kutumia memori kadi.

Bei yake bado haijawekwa wazi ila litakuwa ndio ya juu kuliko haya matoleo mengine na simu itaingia sokoni kuanzia mwezi wa nne.

Bei;

Toleo la bei nafuu ni la Galaxy S10E ambalo litauzwa kuanzia dola 750 za Marekani (Takribani Tsh 1,750,000/= ), Galaxy S10 ni dola 900 ambazo ni takribani Tsh 2,100,000/=. Galaxy S10 Plus ni dola 1,000, takribani Tsh 2,330,000/=).

MPYA

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |