fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Samsung simu Uchambuzi

Uchambuzi wa Samsung Galaxy A2 Core, Uwezo na Sifa. #Simu #BeiNafuu

tecno

Simu ya Samsung Galaxy A2 Core ni simu ya bei nafuu kutoka kampuni ya Samsung. Ni yenye umbo la wastani kwa ukubwa wa inchi 5.

Simu hii inatumia mfumo endeshi wa Android uliorahisishwa (Go Edition). Hili ni toleo jepesi la Android linalohakikisha simu zisizo na uwezo wa juu sana kuweza kuwa na ufanisi mzuri wa utumiaji apps mbalimbali za Android, fahamu zaidi hapa -> Fahamu kuhusu toleo la Android Go.

Samsung Galaxy A2 Core

Simu ya Samsung Galaxy A2 Core

Sifa za simu hii:

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya TFT chenye ukubwa wa inch 5.0
  • Mfumo endeshi wa Android 8.1 Go Edition.
  • Exynos 7870 SoC.
  • RAM ya GB 16 na diski uhifadhi ya GB 1.
  • Kamera ya nyuma yenye megapixel 5 na kamera ya mbele yenye megapixel 5.
  • Betri yenye uwezo wa 2600mAh.
SOMA PIA  Samsung Galaxy S9/S9+ yapokea Android Pie

Simu ya Samsung Galaxy A2 Core

Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, ikiwa pia na huduma za WiFi, Bluetooth na FM Radio kwa ajili ya kusikiliza redio.

tecno

Simu hii ina sehemu ya kuchomeka earphones, sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0 na huja katika rangi nne ambazo ni Nyeusi (Black), Bluu (Blue), Nyekundu (Red) na Dhahabu (Gold).

SOMA PIA  Samsung kuondoa 'Earphone Jack'

Je una mtazamo gani juu ya simu hii? Je ni simu gani nyingine inakuvutia zaidi kutoka Samsung na ungependa tuichambue?

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania