Je tayari umeshatumia app ya TrueCaller na sasa unajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa kabisa namba yako ya simu na data zingine kutoka kwenye app ya TrueCaller?
Leo tutakufundisha hivyo, tutakuelekeza ata kama wewe bado haujajiunga na app hiyo ila namba yako tayari imeunganisha kwenye mfumo huo.
Soma pia – App ya TrueCaller inafanyaje kazi?
Jinsi ya kuondoa namba yako kwenye mfumo huu ina njia mbili na inategemea kama tayari ulijiandikisha kwenye huduma hii au haujajiandikisha ila kutokana na mtu anayetumia app hii kuwa na namba yako basi na taarifia zako zimeingizwa.

Kwa wale wenye akaunti za TrueCaller
- Fungua app ya TrueCaller, nenda kwenye alama ya nukta tatu upande wa kushoto juu.
- Kisha nenda Settings, kisha About, na hapo utaona chaguo la ‘Deactivate Account’ yaani futa akaunti…
- Ata ukishafuta akaunti yako, yaani ‘deactivate account’ bado namba yako inaweza kuwa kwenye data za TrueCaller. Na hapa ndio inabidi uchukue hatua inayofanana na wale ambao hawana akaunti ya TrueCaller.
Kwa wale wasio na akaunti ya TrueCaller au wamefuta/deactivate akaunti zao
- Hatua inayofuata ni kuondoa namba kwenye mfumo wa kompyuta (servers) za huduma ya TrueCaller.
- Nenda kwenye tovuti ya TrueCaller huduma ya kuondoa namba (Unlist)
- Ukifika hapa andika namba yako ya simu, chukua hatua za kuonesha ya kwamba wewe ni binadamu (captcha) na kisha bofya ‘Unlist’
Kwa wengi kuna faida flani katika huduma hii, mfano kufahamu jina la mtu anayekupigia kabla ya kupokea inaweza ikawa muhimu sana kikazi. Vipi wewe unamtazamo gani juu ya huduma ya TrueCaller?
Soma pia – App ya TrueCaller inafanyaje kazi?