fbpx

Bei ya Samsung Galaxy S10, S10 Plus na S0e Tanzania yatangazwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Je ushajiuliza kuhusu bei ya Samsung Galaxy S10? Samsung Tanzania wameweka wazi bei ya simu za Samsung Galaxy S10, hii ikiwa ni pamoja na kuanza kupokea pesa za wanaoweza kulipia mapema (Pre-order).

Simu za Galaxy S10 zilizotambulishwa rasmi wiki hii zimesifika sana kwa teknolojia na ubora wake ingawa kwenye suala la bei zinazidi kujiweka mbali na watumiaji wasio na bajeti kubwa ya kifedha kwa ajili ya simu. Unaweza kusoma uchambuzi hapa -> Uchambuzi wa Samsung Galaxy S10

bei ya samsung galaxy s10

Muonekano: Samsung Galaxy S10e, Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus

Pia watatoa zawadi kwa wanunuaji wa kwanza ambao kwa kiasi kikubwa watakuwa ni wale watakaoweza kufanya malipo ya kabla (preorder) mapema zaidi.

INAYOHUSIANA  Instagram yazindua IGTV. IGTV ni nini?

Bei hizo ni kama ifuatavyo;

  • Samsung Galaxy S10 – Tsh 2,435,000/=
  • Samsung Galaxy S10e – Tsh 2,022,00/=
  • Samsung Galaxy S10 Plus – Tsh 2,715,000/= (GB 128) wakati toleo la GB 512 la Galaxy 10 Plus itakuwa ni Tsh 3,265,000/=

Kwa watu wa kwanza 100 kuweka oda za Galaxy S10 au Galaxy S10e watapata na earphones za bila waya – Galaxy buds bure. Kumbuka Galxy buds moja kawaida huwa inauzwa Tsh 465,000/=.

INAYOHUSIANA  Tanzania Kushirikiana na Toshiba katika Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi

Kwa watu wa kwanza 50 kuweka oda za Galaxy S10 Plus watapata saa ya Galaxy Sport yenye thamani ya Tsh 465,000/=.

Watu wenye nia ya kulipia mapema ili kuweza kupata ofa hizi wanatakiwa kulipia kupitia maduka ya Tigo na yale ya Samsung sehemu yeyote nchini.

Soma uchambuzi wa matoleo yote ya Samsung Galaxy S10 hapa -> Uchambuzi wa Samsung Galaxy S10

Vipi unaonaje hizi bei? 🙂

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.